Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hababuu awachimba mkwara Wasudani

HABABUU Pict

Muktasari:

  • KVZ itamenyana na Al Hilal Julai 29 ikiwa inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika Kombe la CECAFA Kagame 2026, huku Hababuu akisisitiza kuwa timu yake bado haijakata tamaa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

KOCHA wa KVZ ya Zanzibar, Hababuu Omar amesema hana hofu na mchezo ujao dhidi ya Al Hilal ya Sudan akiamini kikosi chake kitaonyesha sura tofauti kutokana na mechi hiyo kuchezwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele wenye nyasi bandia.

Hababuu amesema mazingira hayo yanakipa kikosi chake faida kwa kuwa asilimia kubwa ya viwanja vinavyotumika kwenye Ligi Kuu ya Zanzibar vina nyasi bandia, hivyo wachezaji wamezoea aina hiyo ya uwanja.

“Na fikiri tutakuwa na nafasi nzuri ya kucheza soka letu. Wachezaji wetu wamezoea kucheza kwenye nyasi bandia, hivyo naamini wataonyesha kiwango kizuri zaidi kuliko mechi iliyopita,” amesema kocha huyo.

KVZ ilianza michuano hiyo kwa kupoteza mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Rayon Sports kwenye Uwanja wa Amahoro, matokeo yaliyoifanya kubaki bila pointi.

Hababuu amesema pamoja na kupoteza, wachezaji wake walipambana lakini walikumbana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa Rayon Sports waliojaa uwanjani, hali iliyowafanya kushindwa kucheza kwa utulivu.

“Ilikuwa mechi ngumu kwa sababu ya mazingira na sapoti kubwa ya wenyeji. Pia tuna kikosi chenye wachezaji wengi wapya ambao bado wanaendelea kuzoeana, lakini naamini mchezo ujao watakuwa watulivu zaidi,” ameongeza.

KVZ itamenyana na Al Hilal Julai 29 ikiwa inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika Kombe la CECAFA Kagame 2026, huku Hababuu akisisitiza kuwa timu yake bado haijakata tamaa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.