Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker agoma kushusha tanga katikati ya mawimbi

BARKER Pict


KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker amesema mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara bado ziko wazi licha ya timu hiyo kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, jijini Dar es Salaam.


Matokeo ya dabi hiyo ya Kariakoo iliyochezwa Jumapili, yaliifanya Simba kushindwa kupunguza tofauti ya pointi kati yao na Wananchi hivyo Yanga imeendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 48 huku Wekundu hao wa Msimbazi wakisalia nafasi ya pili na pointi 43.


Zimesalia mechi kumi kwa timu hizo zenye pointi 30 na kila moja inazipigia hesabu kuzikusanya zote, kisha kukaa chini kuangalia nani anazo nyingi katika mbio hizo za ubingwa. Endapo kila moja ikikusanya zote, maana yake Yanga itamaliza kileleni na pointi 78, huku Simba ikiishia 73.

ISAMU 07

Kuhusu mechi ya juzi, Barker amesema Simba walianza vizuri dabi hiyo ya 116 katika ligi wakilenga kujiweka nafasi nzuri ya ubingwa lakini kwa bahati mbaya vijana wake wakapoteza umakini baada ya kuwa mbele kwa mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Libasse Gueye na Clatous Chama.

“Tulianza vizuri sana mchezo, tulikuwa tunashambulia na kushinda mipira mingi katikati, tukawaweka presha kubwa na hilo lilitusaidia katika dakika 10 za kwanza,” amesema kocha huyo ambaye ameipa Simba ubingwa wa Kombe la Muungano siku chache zilizopita.

ISAMU 06

Alifafanua kwa kusema mabao hayo yalitokana na mpango kushambulia kwa kasi.

“Tulikuwa wazuri kwenye mikimbio ya haraka katika maeneo yote ya uwanja, tulijua kwa kufanya hivyo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuimaliza mechi mapema na tulifanikiwa kupata mabao hayo,” amesema kocha huyo raia wa Afrika Kusini.

Hata hivyo, alikiri kupoteza umakini kulibadilisha mwelekeo wa mchezo huo.

ISAMU 05

“Baada ya kufunga bao la pili, hatukuendelea na ile kasi na tukawapa nafasi wapinzani wetu, lakini pamoja na hilo nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu na bado tunayo nafasi kwenye mbio za ubingwa,” amesema.

Katika mechi zilizobaki, Simba inatarajiwa kukutana na JKT Tanzania, Tanzania Prisons, Mashujaa, Coastal Union, Dodoma Jiji, Pamba, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Singida Black Stars na KMC.

ISAMU 04

Kuhusu mechi hizo, Barker amesema: "Hatuna tena nafasi ya kudondosha pointi, tunatakiwa kupambana na kufanya vizuri katika michezo yote iliyosalia, halafu mwishowe tutaona nini kitatokea, hatuwezi kukata tamaa kwa sababu huu ni mpira na lolote linaweza kutokea."

Kwa upande wa Yanga, ratiba yao iliyosalia ni dhidi ya KMC, kisha Coastal Union, Dodoma Jiji, Singida Black Stars na Namungo kabla ya kukutana na Mashujaa, Fountain Gate, Azam, TRA United na kumalizia na JKT Tanzania.


ISHU YA OURA

Barker alieleza pia kwa nini hakumtumia kabisa nyota wake Anicet Oura ambaye alikuwa gumzo katika dabi ya duru la kwanza kabla ya kuumia katika fainali ya Kombe la Muungano, Zanzibar.

"Nadhani tuliongea kuhusu hilo, majeraha yake sio makubwa na alikuwa katika nafasi ya kutumika lakini tuliamua kumpumzisha ili atumike katika michezo mwingine, kumtumia ingeweza pengine kusababisha shida kubwa zaidi," amesema kocha huyo.