Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodi ya Ligi yachomoa Milioni 10 Simba

Muktasari:

  • Jabaar alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kwenye mchezo huo uliopigwa Agosti 19, ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

BODI ya Ligi Kuu imeitoza Simba kiasi cha Sh 10 Milioni kwa adhabu mbili ya kwanza kiungo wake Ibraheem Jabaar aliyekamuliwa faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji, Abdulkarim Iddy na nyingine ikienda kwa mashabiki.

Jabaar alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kwenye mchezo huo uliopigwa Agosti 19, ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ya Agosti 22, adhabu hiyo imetolewa chini ya Kanuni ya 42:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa Wachezaji.

Lakini kwa Simba imetozwa kiasi hicho kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa waamuzi wakati wa mapumziko hali iliyofanya waamuzi hao kushindwa kutumia vyumba vya kubadilishia nguo.

Huu umekuwa muendelezo kwa mashabiki wa Simba kufanya vurugu uwanjani, msimu uliopita, Simba iliwahi kutozwa faini ya Sh10 milioni baada ya mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi walipokuwa wakitoka uwanjani baada ya mchezo wa Pamba Jiji 1-1 Simba, Machi 19, 2026.

Februari 25, 2026 mashabiki wa Simba walikuwa wamefanya tukio kama hilo katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ambapo walimrushia chupa mchezaji wa Dodoma Jiji, William Edgar.

Katika taarifa hiyo hiyo ya Agosti 22, TPLB imemfungia pia Mathew Tegisi wa Singida Black Stars michezo mitatu na kumtoza Sh5 milioni kwa kumpiga kiwiko Salehe Seif wa Kagera Sugar.

Mwamuzi wa kati Tatu Malogo naye ameadhibiwa kwa kosa la kushindwa kuonyesha ufanisi katika mchezo uliotokana na kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu, adhabu iliyotolewa chini ya Kanuni ya 43:1(1.8) kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

TPLB imezikumbusha timu kwamba ni Kocha Mkuu au kiongozi mwingine wa juu kwenye benchi mwenye mamlaka ya kuwasilisha ombi la marejeo ya tukio kwenye teknolojia ya FVS.

Kwa mujibu wa Bodi hiyo, mchezaji ataonekana kukiuka masharti iwapo atamkabili, kumlalamikia au kumshinikiza mwamuzi moja kwa moja kwa lengo la kuomba marejeo ya FVS, na anaweza kuadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62.