Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Equity Waitara Trophy 2026 kukutanisha gofu, maisha na fursa za kifedha

Muktasari:

  • Mashindano hayo yatafanyika Septemba 19, 2026 katika Klabu ya Gofu ya TPDF Lugalo, Dar es Salaam, na yameandaliwa kwa heshima ya Jenerali Mstaafu George Waitara, mwanzilishi wa klabu hiyo.

Benki ya Equity imezindua Equity Waitara Trophy 2026, mashindano yanayolenga kuwakutanisha wapenzi wa mchezo wa gofu, viongozi wa biashara, wajasiriamali na wataalamu mbalimbali huku yakitoa fursa ya kujenga uhusiano, mitandao na ustawi wa kifedha.

Mashindano hayo yatafanyika Septemba 19, 2026 katika Klabu ya Gofu ya TPDF Lugalo, Dar es Salaam, na yameandaliwa kwa heshima ya Jenerali Mstaafu George Waitara, mwanzilishi wa klabu hiyo.

Udhamini wa mashindano hayo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuimarisha uhusiano na wateja wa hadhi ya juu pamoja na jamii pana ya wapenzi wa gofu nchini Tanzania.

Akizungumza kuhusu udhamini huo, mkuu wa wa masoko wa benki hiyo Shumbana Walwa, amesema gofu ni zaidi ya mchezo kwani hujenga uhusiano, nidhamu na fursa za ukuaji.

“Golf ni zaidi ya mchezo. Ni sehemu ya maisha inayojengwa katika malengo, nidhamu, mahusiano na ukuaji. Kupitia Equity Waitara Trophy 2026, tunataka kuwa karibu zaidi na jamii ya golf nchini, kushiriki shauku yao na kutengeneza uzoefu unaowaunganisha ndani na nje ya uwanja,” amesema Walwa.

“Wateja wetu wana malengo yanayokwenda zaidi ya huduma za kawaida za kibenki. Wanawekeza, wanasafiri, wanamiliki na kukuza biashara, wanajenga mali na kuandaa maisha ya baadaye. Kupitia huduma zetu za premium banking na Equity Mastercard World Elite Debit Card, tunataka kuwa mshirika anayeelewa maisha na malengo yao na kuwaunganisha na suluhisho zinazowasaidia kuinua maisha yao na kujenga ustawi wa kifedha,”

Amesema kupitia mashindano hayo, Equity inalenga kuwa karibu zaidi na jamii ya gofu na kuwaunganisha wateja na huduma zinazoendana na maisha na malengo yao ya kifedha.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa jukwaa la kusherehekea mchezo wa gofu, kujenga mitandao na kuimarisha uhusiano kati ya Equity, wateja na wadau mbalimbali nchini.