Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge achekelea sare ya dabi

IBENGE Pict

Muktasari:

  • Juzi Jumapili, Simba ikiwa mwenyeji wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

KOCHA Mkuu wa Azam, Florent Ibenge, amesema sare ya 2-2 baina ya Simba na Yanga ni matokeo mazuri kwao lakini itakuwa faida zaidi endapo wataendelea kushinda mechi zilizosalia.

Juzi Jumapili, Simba ikiwa mwenyeji wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Azam inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 40, ikiwa nyuma ya Simba yenye pointi 43 huku Yanga ikiongoza na 48, zote zikicheza mechi 20.

Kama Azam itafanikiwa kushinda mechi kumi zilizobaki, itamaliza msimu na pointi 70, hivyo inabaki kwa wapinzani wake hao wawili kuwaombea mabaya kwani tofauti yake na Simba ni pointi tatu, huku ikiachwa pointi nane na Yanga.

IBE 01
IBE 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Ibenge amesema amefurahia sare hiyo katika Dabi ya Kariakoo akisema ni matokeo mazuri kwenye malengo ya Azam lakini itakuwa faida zaidi endapo wataendelea kushinda.

Amesema atazungumza na wachezaji kuwakumbusha wanatakiwa kuendelea kushinda ili kutumia faida ya kupunguza tofauti ya pointi kati yao na timu hizo mbili za juu.

"Nimefurahia sare ya dabi ya Simba na Yanga kwa sababu ni matokeo mazuri kwenye malengo ya Azam, yanatupa nafasi nzuri kwenye mbio za juu ya msimamo, faida hii itakuwa kubwa zaidi endapo tutaendelea kushinda michezo yetu ijayo.

"Nitazungumza na wachezaji wangu ili waendelee kushinda na kupunguza tofauti ya pointi kati yetu na timu hizo mbili za juu, licha ya wapinzani wetu kuwa na ubora wa hali ya juu lakini bado tuna nafasi ya kupambana," amesema Ibenge.

IBE 02
IBE 02

Azam leo itaikaribisha Namungo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, wanakutana wakiwa na rekodi ya sare ya 1-1 katika mchezo wa duru la kwanza.

Katika safari ya mechi zao kumi zilizobaki, Azam tayari imemalizana na Simba ikianza na ushindi wa mabao 2-0, kisha 0-0, huku ikitarajiwa kucheza ugenini dhidi ya Yanga Juni 24 mwaka huu. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa matokeo ya 0-0. Hivyo unaweza kusema moja kati ya mechi ngumu na ya kujiuliza ambayo Ibenge amesalia nayo kwenye ratiba ni dhidi ya Yanga.

Mechi zingine ni dhidi ya Namungo (nyumbani), TRA United (ugenini), Pamba Jiji (nyumbani), Tanzania Prisons (nyumbani), KMC (nyumbani), Fountain Gate (ugenini), Mashujaa (nyumbani), Coastal Union (ugenini) na Dodoma Jiji (nyumbani).