Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matthew Tegis afikia rekodi ya Chama

TEGISI Pict

Muktasari:

  • Huyo si mwingine bali ni mshambuliaji wa Singida Black Stars, Matthew Tegis, ambaye amejiweka kwenye orodha ya wachezaji waliofunga hat-trick katika mashindano ya klabu yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kupachika mabao matatu dhidi ya Al Ghazala katika Kombe la Shirikisho Afrika.

SI unakumbuka ile hat trick ya kiungo wa Simba, Clatous Chama aliyofunga wakati timu hiyo inashinda 7-0 dhidi ya Horoya AC katika Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Machi 18, 2023? Sasa imepita miaka mitatu, mchezaji mwingine kutoka Ligi Kuu Bara amefanya hivyo.

Huyo si mwingine bali ni mshambuliaji wa Singida Black Stars, Matthew Tegis, ambaye amejiweka kwenye orodha ya wachezaji waliofunga hat-trick katika mashindano ya klabu yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kupachika mabao matatu dhidi ya Al Ghazala katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Tegis amefunga mabao hayo wakati Singida Black Stars ikishinda 7-1, mechi ya kwanza iliyochezwa juzi Jumapili nchini Sudan Kusini.

Mshambuliaji huyo raia wa Kenya, alifunga mabao hayo dakika ya 20, 23 na 32, akitumia dakika 12 pekee akiwa mchezaji wa tano kupiga hat trick kutoka Ligi Kuu Bara tangu mwaka 2009, huku akiwa wa kwanza kutoka nje ya Simba na Yanga kufanya hivyo.

MOMA 01

Mchezaji wa kwanza kutoka Ligi Kuu Bara kufunga hat trick ni mshambuliaji Mkenya, Boniface Ambani akiwa Yanga, alifunga mabao manne katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Etoile d’Or ya Comoros, Januari 31, 2009.

Akafuatia Mrisho Ngassa aliyefanya hivyo mara tatu. Alianza kufunga mabao manne katika ushindi wa Yanga wa 6-0 dhidi ya Etoile d’Or, Februari 15, 2009, kisha mwaka 2014, alipofunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 ilioupata Yanga dhidi ya Comorozine, Februari 8, kabla ya kufanya hivyo tena katika ushindi wa 5-2 dhidi ya timu hiyo Februari 15.

Wa tatu alikuwa Fiston Mayele akiwa na kikosi cha Yanga mwaka 2022, alifunga hat-trick dhidi ya Zalan FC katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Septemba 10, na akarudia katika mchezo wa marudiano Septemba 17.

Mwaka 2023, Clatous Chama akawa mchezaji wa nne kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara kufunga hat-trick mashindano ya CAF akifanya hivyo katika ushindi wa Simba wa 7-0 dhidi ya Horoya AC, Machi 18.

MOMA 02

Sasa mwaka huu 2026, Tegis ameongeza jina lake kwenye historia hiyo akiwa na Singida Black Stars, akifanya hivyo katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ghazala.

Akizungumzia hilo, Tegisi amesema: “Hat-trick yangu ya kwanza kimataifa lakini nimefurahia na nawashukuru wenzangu tumekuwa pamoja na kufanikisha mimi kufunga idadi hiyo ya mabao.”


REKODI YA HAT TRICK

Hat-trick hiyo imemwingiza Tegis kwenye orodha ambayo ina mastaa mbalimbali wa soka la Afrika waliofanya tukio hilo katika mashindano ya CAF tangu mwaka 2009.

Kwa mujibu wa rekodi hiyo, historia inaanzia Januari 31, 2009, ambapo Mus tapha Allaoui wa FAR Rabat alifunga hat-trick dhidi ya Sporting Clube da Praia katika ushindi wa mabao 6-1.

Siku hiyo hiyo, Mkenya Boniface Ambani, akiwa Yanga, alifunga mabao manne katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Etoile d’Or ya Comoros.

Tanzania iliendelea kuonekana kwenye rekodi hiyo muda mfupi baadaye, kupitia Mrisho Ngasa, aliyefunga mabao manne katika ushindi wa Yanga wa 6-0 dhidi ya Etoile d’Or, Februari 15, 2009.

MOMANYI Pict

Ngasa hakuishia hapo. Mshambuliaji huyo alirudia kufunga hat-trick katika mashindano ya CAF mwaka 2014, alipofunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 ilioupata Yanga dhidi ya Comorozine, Februari 8, kabla ya kufanya hivyo tena katika ushindi wa 5-2 dhidi ya timu hiyo Februari 15.

Kabla ya hapo, rekodi hiyo ilikuwa imeendelea kuongezeka kwa majina kutoka mataifa mbalimbali, akiwamo Jonas Sakuwaha wa Zambia, Dioko Kaliyutuka wa TP Mazembe, Joka wa Atletico Petroleos Luanda, Hassan Tair wa Raja Casablanca na Adama Bakayoko wa ASEC Mimosas.

Mwaka 2015, Mbwana Samatta aliweka jina lake kwenye rekodi hiyo akiwa TP Mazembe, alipofunga mabao matatu dhidi ya Moghreb Tétouan katika ushindi wa 5-0, Septemba 12.

Mwaka 2018 ulikuwa na matukio kadhaa. Hamid Ahaddad alifunga mabao matano, huku Simon Msuva naye akifunga hat-trick katika ushindi wa Difaa El Jadidi wa 10-0 dhidi ya Sport Bissau e Benfica.

Kisha mwaka 2022, Tanzania ikaibuka tena kwenye orodha hiyo kupitia Fiston Mayele akiwa Yanga, aliyefunga hat-trick dhidi ya Zalan FC katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Septemba 10, na akarudia tena katika mchezo wa marudiano Septemba 17.