Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtihani wa kwanza wa Moalin dhidi ya Coastal upo hapa!

MOALLIN Pict

Muktasari:

  • Katika mkutano na wanahabari, Kocha Moalin, aliyepokea kijiti cha mtangulizi wake, Pedro Goncalves aliyefutwa kazi baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda bao 1-0 dhidi ya KMC, amesema:

KUTOKANA na Yanga kupishana na Simba kwa pointi tano, ina kazi ya kuhakikisha inashinda mechi dhidi ya Coastal Union ili kuendelea kujiwekea mazingira ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara msimu huu, kama anavyosema kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Abdihamid Moalin.

Katika mkutano na wanahabari, Kocha Moalin, aliyepokea kijiti cha mtangulizi wake, Pedro Goncalves aliyefutwa kazi baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda bao 1-0 dhidi ya KMC, amesema:

“Falsafa yangu ni kuhakikisha timu inatawala mpira na kuumiliki, kuhakikisha tunamentain viwango bora vya wachezaji, hivyo tupo tayari kwa ajili ya mechi hiyo.”

MOA 01

Moalin aliyeambatana na kipa Abdultwalib Mshery aliyesema: “Kila kocha ana mbinu zake ambazo tutatakiwa kuzifuata, lakini Kocha Moalin tulikuwepo naye, amerejea kwa mara nyingine, lakini kuhusu mechi dhidi ya Coastal, tumejipanga kwa ushindi.”

Wakati huo huo, kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias, amesema: “Natarajia mechi itakuwa ngumu na ya ushindani, tayari tumepata muda wa siku mbili kuboresha na kuimarisha baadhi ya maeneo ili kuhakikisha tunafanya vizuri.”

Katika mechi 21, Yanga imeshinda 15, sare sita, inamiliki mabao 47, imefungwa mabao matano na ina pointi 51, huku Coastal Union iliyopo nafasi ya 12, katika mechi 21 ilizocheza, imeshinda tano, sare saba, imefungwa tisa, imefunga mabao 20, imeruhusu mabao 26 na ina alama 22.

MOA 02

Ukiachana na hilo, kwa takwimu za wachezaji, mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube, ana mabao tisa. Wanaomfuatia ni Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua, kila mmoja akiwa na mabao saba. Upande wa Coastal Union, Maabad Maulid na Shiza Kichuya kila mmoja anamiliki mabao manne, huku Cleophace Mkandala akiwa na mabao matatu.

Mechi nyingine itakayopigwa leo ni kati ya JKT Tanzania na Mbeya City na kocha msaidizi wa Maafande hao, Raymond Dotto, amesema: “Mbeya City ni timu ngumu, lakini plan zetu ni kushinda ili kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya nafasi za juu katika msimamo wa ligi.”

MOA 03

Kwa upande wa kiungo wa timu hiyo, Ally Hussein Msengi, amesema: “Kama wachezaji, maandalizi yetu yalikuwa mazuri, makocha wametupa mbinu, tupo tayari kwa mapambano.”

Wakati huo huo, kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga, amesema: “Itakuwa mechi ngumu, tunahitaji ushindi kwani tupo nafasi mbaya katika msimamo wa ligi, lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Kikubwa ni kuepuka kufanya makosa yatakayotugharimu.”

MOA 04

Kabla ya matokeo ya mechi hiyo, JKT Tanzania ipo nafasi ya tano. Katika mechi 21, imeshinda nane, sare nane, imefungwa tano, imefunga mabao 21, imefungwa mabao 21 na ina alama 32. Mbeya City ipo nafasi ya 14 na katika mechi 21 imeshinda tano, sare sita, imefungwa 10, imefunga mabao 18, imetikiswa nyavuni mara 31 na ina pointi 21.

Kinara wa mabao kwa JKT Tanzania ni Saleh Karabaka mwenye mabao saba, akifuatiwa na Valentino Mashaka pamoja na Paul Peter, kila mmoja akiwa amefunga mabao matano. Kwa upande wa Mbeya City, wanaoongoza kwa mabao ni Vitalis Mayanga na Adilly Buha, kila mmoja akiwa na mabao matatu.

MOA 05

Mechi nyingine ni ya Singida Black Stars iliyopo nafasi ya nne. Katika mechi 21, imeshinda tisa, sare tano, imefungwa saba, imefunga mabao 25, imefungwa mabao 23 na ina alama 32.

Timu hiyo itakutana na Mtibwa Sugar iliyopo nafasi ya 11, ambayo imecheza mechi 21, ikishinda tano, sare nane, kufungwa nane, imefunga mabao 16, imeruhusu mabao 25 na ina pointi 23.

Kocha wa Singida Black Stars, Muhibu Kanu, amesema: “Timu ipo tayari kukabiliana na Mtibwa, tunahitaji ushindi ili kuhakikisha tunakaa nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi. Hiyo itatusaidia kufikia ndoto zetu za kucheza michuano ya kimataifa.”

MOA 06

Nyota anayeongoza kwa mabao kwa upande wa Singida Black Stars ni Mossi Ndumbaro mwenye mabao matano, akifuatiwa na beki Ibrahim Imoro mwenye mabao matatu na kiungo Emmanuel Keyekeh mwenye mabao mawili.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, wanaoongoza kwa mabao ni Ismail Mhesa na Magata Charles, kila mmoja akiwa amefunga mabao matatu.