Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yafuata mashine mpya Uganda

SIMBA Pict


MABOSI wa Simba wameanza mchakato wa kuboresha kikosi hicho msimu ujao na miongoni mwa nyota wakubwa wanaoangaliwa ni kiungo mshambuliaji wa Vipers ya Uganda ambaye ndiye mchezaji bora wa msimu wa 2025-2026 (MVP), Abdulkarim Watambala.


Simba imekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu ikiwa hadi sasa imepishana na vinara wa ligi Yanga kwa tofauti ya pointi mbili huku msimu ukiwa umebakiza michezo mitano tu kwa kila timu ili umalizike.


Taarifa kutoka Uganda zinaeleza mabosi wa Simba wameanza kumfuatilia kiungo huyo kimyakimya kwa ajili ya kujiunga nao msimu ujao, ikielezwa ni mbadala wa nyota, Naby Camara raia wa Guinea, ambaye huenda akaondoka kwenye klabu hiyo mwisho wa msimu huu kutokana na kukosa nafasi ya uhakika kikosini.

SIMB 01

Camara aliyejiunga na timu hiyo Agosti 14, 2025, akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Al-Waab SC ya Qatar, licha ya kucheza nafasi mbalimbali uwanjani ila ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi la kikosi hicho cha Kocha, Steve Barker.

Nyota huyo anayemudu kucheza beki wa kushoto na kiungo mshambuliaji kwa ufasaha, amekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara, jambo linaloweza kumfungulia milango ya kuondoka, licha ya kubakisha mkataba wa mwaka mmoja.

Taarifa kutoka Uganda zinaeleza miongoni mwa nyota wanaoangaliwa zaidi kuziba nafasi ya Camara ni Watambala ambaye ameonyesha kiwango bora na kikosi cha Vipers, kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uganda kwa msimu wa 2025-2026.

SIMB 03

Hata hivyo, taarifa hizo zinaeleza mabosi wa Vipers wanahofia huenda nyota huyo akaondoka baada ya timu mbalimbali pia kuonyesha nia ya kumuhitaji nje ya mipaka ya Uganda, huku Simba ikipewa nafasi licha ya kutokamilika kwa taratibu zote.

Katika Ligi Kuu ya Uganda msimu wa 2025-2026, Watambala amechangia mabao 16 ya Vipers, baada ya kufunga 12 na kuasisti manne kwenye mechi 28, alizocheza kati ya 30, jambo lililomuwezesha kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa nchi hiyo (MVP).

Watambala alishinda tuzo hiyo kutokana na kiwango bora alichokionyesha na Vipers, akiwashinda Frank Ssebufu na Raymond Barasa Mangoli wanaocheza wote SC Villa, Ivan Ahimbisibwe wa KCCA na Ambrose Kigozi anayecheza kikosi cha Entebbe UPPC.

SIMB 02

Mbali na kutwaa tuzo, ila Watambala ameiwezesha Vipers kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uganda msimu wa 2025-2026, baada ya timu hiyo kumaliza vinara na pointi 67, ikishinda mechi 19, sare 10 na kupoteza moja, ikifunga mabao 55 na kuruhusu 17.

Kwa sasa kiungo mshambuliaji Allan Okello ndiye anatajwa kuwa mchezaji mahiri zaidi kwenye Ligi Kuu Bara akiwa ameshafunga mabao 11 naye alijiunga na Yanga akitokea Vipers mwanzoni mwa mwaka huu, jambo ambalo linaonyesha kuwa timu hiyo ina vipaji vya kutosha.