Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars imebakiza moja kutinga robo fainali WAFCON

TWIGA Pict

Muktasari:

  • Tanzania ina kibarua dhidi ya Burkina Faso kwenye mechi ya pili ya kundi B itakayopigwa Juali 31 saa 5 usiku katika Uwanja wa Larbi Zaouli Stadium, Casablanca.

USHINDI wa kihistoria wa mabao 2-1 wa Tanzania dhidi ya Afrika Kusini umeifanya Twiga Stars kubakiza mechi moja tu ili kuandika historia nyingine katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.

Tanzania ina kibarua dhidi ya Burkina Faso kwenye mechi ya pili ya kundi B itakayopigwa Juali 31 saa 5 usiku katika Uwanja wa Larbi Zaouli Stadium, Casablanca.

Iwapo Tanzania itaibuka na ushindi katika mchezo huo, itafikisha pointi sita, ambazo zitakuwa zinatosha kuihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali moja kwa moja bila kusubiri matokeo ya mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Ivory Coast.

Huo utakuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa kwa Twiga Stars, ambayo katika ushiriki wake wa kwanza mwaka 2010 ilipoteza mechi zote tatu za makundi, huku mwaka 2024 ikimaliza na pointi moja pekee.

Hata hivyo, Burkina Faso si timu ya kubezwa. Ingawa haina historia kubwa kama Afrika Kusini, imeendelea kupiga hatua katika soka la wanawake na imeonyesha ushindani mkubwa katika safari ya kufuzu WAFCON 2026.

Burkina Faso inashiriki WAFCON kwa mara ya tatu kama ilivyo Stars katika historia yake, baada ya kushiriki mwaka 2014 na 2024. Katika matoleo yote mawili haikuwahi kuvuka hatua ya makundi lakini ina mchanganyiko wa wachezaji vijana na wenye uzoefu.

Katika historia ya mashindano hayo, Burkina Faso haijawahi kufuzu robo fainali, jambo linaloifanya mechi dhidi ya Tanzania kuwa muhimu kwao kama ilivyo kwa Twiga Stars. Endapo itapoteza mchezo huo, nafasi yake ya kusonga mbele inaweza kuwa finyu kutegemeana na matokeo ya mechi nyingine za kundi.

Kwenye rekodi Tanzania na Burkina Faso hazijawahi kukutana kwenye WAFCON, hivyo mchezo wa Julai 31 utakuwa wa kwanza katika historia ya michuano hiyo. Hilo linaongeza ugumu wa kutabiri matokeo kwani hakuna timu inayofahamu vizuri mbinu za mwenzake.