Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita Kipa Bora Zanzibar  yanoga

KIPA Pict

Muktasari:

  • Kipa wa timu ya Uhamiaji, Ahmed Ali na Arjif Ali wa Polisi, wanaendelea kuongoza jahazi hilo wakiwa wamejikusanyia ‘clean sheet’ nne kila mmoja ambapo Ahmed alizipata kwenye mechi dhidi ya Mwenge, Wembe, Raskazone na Fufuni.

MBIO za kuwania tuzo ya Kipa Bora msimu wa 2026-2027 zipo kwenye hatua ya kuvutia zaidi baada ya matokeo kuweka safu ya makipa hao katika ushindani wa karibu.

Kipa wa timu ya Uhamiaji, Ahmed Ali na Arjif Ali wa Polisi, wanaendelea kuongoza jahazi hilo wakiwa wamejikusanyia ‘clean sheet’ nne kila mmoja ambapo Ahmed alizipata kwenye mechi dhidi ya Mwenge, Wembe, Raskazone na Fufuni.

Kwa upande wake Arjif alizipata kwenye mechi ya KVZ, Mwenge, Mafunzo na Mlandege, hali hiyo imeleta shinikizo kwa timu zao kuendeleza nidhamu ya ulinzi katika mechi zinazofuata.

​Licha ya uongozi wa wawili hao, Kipa wa KVZ, Hamad Ubwa, Rashid Khamis wa Muembe Makumbi pamoja na Juma Haji wa Raskazone wapo karibu baada ya kila mmoja kuwa na tatu.

Pengo la mechi moja pekee kati ya hao wawili linafanya vita hiyo kuwa ya wazi na isiyotabirika, kosa dogo kutoka kwa makipa wa juu linaweza kubadilisha upepo wa msimamo wakati wowote.

Hamad Ubwa ambaye alipata tuzo hiyo msimu wa 2025-2026, akiwa na cleansheet 12 katika mechi 25 alizocheza akiitumikia timu ya Mlandege iliyomaliza msimu nafasi ya nne akifuatiwa na Ahmed Issa wa JKU akiwa nazo 10 kwa mechi 23, ambaye kwa sasa yupo timu ya Coastal Union.

Kipa huyo aliyejiunga na KVZ amepata cleansheet hizo kwenye mechi ya Fufuni, Raskazone na Mlandege, Juma Haji akipata kwa KMKM, Mafunzo na Fufuni huku Rashid akipata kwenye mechi ya Fufuni, Mafunzo na Mwenge.