Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraza: Ubingwa? Ebu subirini kwanza!

BARAZA Pict

Muktasari:

  • Pamba jana jioni ikiwa nyumbani CCM Kirumba, jijini hapa ilipata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya KMC na kuifanya ikwee hadi kileleni kwa kufikisha pointi 15 baada ya kushinda nne, sare tatu, na kupoteza moja katika mechi nane ilizocheza ikifunga mabao 11 na kufungwa sita.

LICHA ya kikosi cha Pamba Jiji kufanya vizuri hadi sasa katika mechi nane za mwanzo za Ligi Kuu Bara, Kocha Francis Baraza amegoma kuiweka timu hiyo kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

Pamba jana jioni ikiwa nyumbani CCM Kirumba, jijini hapa ilipata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya KMC na kuifanya ikwee hadi kileleni kwa kufikisha pointi 15 baada ya kushinda nne, sare tatu, na kupoteza moja katika mechi nane ilizocheza ikifunga mabao 11 na kufungwa sita.

Akizungumza jijini hapa baada ya mechi hiyo, kocha Baraza ambaye ni raia wa Kenya, amesema anashukuru kwa kile walichonacho kwa sasa mkononi, lakini hawataki kutangaza vita mapema.

Baraza amesema ni vyema waendelee kukusanya pointi katika mechi zijazo ili hata ligi ikimalizika wawe katika nafasi nzuri na kama ni ubingwa ukija hawataukataa.

BARA 01

“Ikipatikana tutakwenda katika ubingwa, lakini sasa hivi mechi nane tunacho kitu mkononi, wale hawajacheza wamecheza mechi chache hawana mkononi,” amesema Baraza na kuongeza;

“Mimi najivunia hizo zangu ambazo ninazo mkononi, ninazo pointi 15 ni kuweza kusukuma tu ikipatikana kuwa tunapata nafasi ya kusonga tutasogea tu, lakini wacha tuibe kimya kimya tusioneshe watu kuwa tunakuja.”

Baraza aliwapongeza wachezaji kwa kuendelea kupambana na kufuata maelekezo anayowapa mazoezini, huku akiwataka kutoridhika mapema.

“Vijana nafikiri kuna kitu wanaonesha na mimi mwenyewe nimeridhika pia kwa sababu tumekuwa tukikosolewa tunafunga mabao machache,” amesema Baraza na kuongeza; “Niliwaambia nyumba haijengwi na tofali moja kwa hiyo sasa nyumba imejengeka. Ushindi wa leo siwezi kuwadharau KMC kwasababu wamecheza vizuri na waetuonesha kitu.”

Kocha huyo wa zamani wa Biashara United, Kagera Sugar na Dodoma Jiji, aliimwagia sifa safu yake ya beki kwa kufanya kazi nzuri na kuzima mashambulizi ya wachezaji wa KMC, huku ikilinda ushindi huo mnono.

BARA 02

“Nitapongeza safu yangu ya ulinzi kutokana na maelekezo tuliyopeana, mana’ke haikuwa rahisi KMC walikuja mara nyingi golini kwetu lakini mabeki na timu nzima wamefanya jambo zuri na tutajaribu kuendelea pale tulipoishia tujaribu kusukuma tena,” amesema Baraza.

Hata hivyo, Mlezi wa timu hiyo, Said Mtanda akifurahia matokeo juzi katika Uwanja wa CCM Kirumba amesema kwa kifupi; “Pamba bingwa.”

Mtanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amesema timu hiyo inafanya vizuri kwa sababu uongozi umetimiza wajibu wake kwa kujifunza makosa ya msimu uliopita na kufanya usajili mzuri.

“Kila nafasi katika kikosi kuna wachezaji zaidi ya wawili ambao wanaweza kucheza muda wowote. Hakuna mchezaji anayedai tumewapa motisha zao Sh10 milioni baada ya ushindi dhidi ya Fountain Gate na kabla ya kucheza tena watakabidhiwa motisha ya ushindi wa leo (juzi),” amesema.

Pamba inatarajiwa kusafiri kwenda Mbeya kukabiliana na Tanzania Prisons katika mechi ijayo iliyopangwa kupigwa Desemba 6 kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini humo.