Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakenya kuipa makali Coastal Union

WAKENYA Pict

Muktasari:

  • Coastal Union haikuwa na mwanzo mzuri chini ya aliyekuwa Kocha Mohamed Muya kabla ya kumvuta kikosini Fikiri Elias aliyeihitimisha msimu timu hiyo ikishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

BAADA ya kutema nyota saba, Coastal Union imesema inaendelea kusuka upya kikosi chake ikitambia ubora wa benchi lake la ufundi ikiahidi msimu ujao kuitafuta nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi, huku katika maandalizi yao, imepanga kucheza mechi za kirafiki dhidi ya FC Leopard na Shabana FC kutoka Ligi Kuu ya Kenya.

Coastal Union haikuwa na mwanzo mzuri chini ya aliyekuwa Kocha Mohamed Muya kabla ya kumvuta kikosini Fikiri Elias aliyeihitimisha msimu timu hiyo ikishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Ligi Kuu msimu wa 2026-2027 inatarajia kuanza Agosti 14, 2026 ambapo Wagosi hao wa Kaya, wanatarajia kufungua pazia kwa kuwakaribisha Mashujaa, Agosti 15, mchezo ukipigwa Mkwakwani jijini Tanga.

Hadi sasa timu hiyo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1988, imeshaweka wazi kuachana na nyota saba ikiwa ni Yassin Mustapha, Jonathan Manyanya, Abdulkarim Segeja, Abdalah Denis, George Wawa, Christopher Ochumu na Wilbol Maseke.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Ayoub Mchomvu, aliliambia Mwanaspoti kuwa baada ya kutema nyota saba, sasa wataanza kushusha mastaa wapya kulingana na mapendekezo ya kocha na mahitaji ya timu kwa ujumla.

Amesema hadi sasa Coastal Union inaendelea na kambi yake tangu Julai 20, 2026 ambapo kuanzia Agosti 1, watajificha mkoani Mara watakapohitimishia maandalizi rasmi ya kujiandaa na msimu ujao.

“Tukiwa huko Shirati wilayani Rorya mkoani Mara, tutacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya FC Leopard na Shabana FC za ligi kuu nchini Kenya, ambapo tunaamini kambi ya siku 11 huko, itatupa kitu bora.

“Kimsingi tumejipanga kuhakikisha msoto tulioanza nao kwa msimu uliopita wa kukosa matokeo mazuri, hatutaki tuyarudie ndio maana tumembakiza kocha wetu apange kikosi na matarajio ni kusaka nafasi nne za juu,” alitamba Mchomvu.

Amesema wapo wachezaji ambao wanaendelea na mazungumzo nao ili kuungana na wenzao waliobaki kikosini na kutokana na mipango iliyopo watamalizana nao mapema ili kuendelea na maandalizi.