Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anthony Edwards aamriwa kulipa Sh44.8 Milioni kila mwezi kwa matunzo ya watoto Wake

Muktasari:

  • Majukumu ya kifedha ya Edwards yanayohusiana na watoto wake yameendelea kuongezeka baada ya jaji mmoja wa Minnesota kumuamuru nyota huyo wa NBA kulipa Dola 14,000 kila mwezi kwa ajili ya mtoto wake wa kiume, Amir.

NEW YORK, MAREKANI; NYOTA wa Minnesota Timberwolves, Anthony Edwards ameamriwa kulipa Dola 14,000 (zaidi ya Sh36.4 milioni) kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto kiasi ambacho kinaongezeka juu ya malipo mengine ya Dola 3,222 (zaidi ya Sh8.4 milioni) katika kesi tofauti.

Majukumu ya kifedha ya Edwards yanayohusiana na watoto wake yameendelea kuongezeka baada ya jaji mmoja wa Minnesota kumuamuru nyota huyo wa NBA kulipa Dola 14,000 kila mwezi kwa ajili ya mtoto wake wa kiume, Amir.

Uamuzi huo mpya, unaomhusisha Edwards na mpenziwe Alexandria Descroches umezingatia kwa kiasi kikubwa kipato cha nyota huyo wa Minnesota Timberwolves. Nyaraka za mahakama zilizoonwa na TMZ zinaonyesha kuwa ana kipato cha karibu Dola 4.8 milioni kwa mwezi, wakati Descroches aliripoti kipato cha takribani Dola 1,016 kwa mwezi.

Uamuzi mpya wa Mahakama ya Minnesota unamtaka Edwards kumlipa Descroches Dola 14,000 kila mwezi kwa ajili ya mtoto wao Amir, aliyezaliwa 2023. Kiasi hicho ni kikubwa zaidi ya kiwango cha msingi cha matunzo ya mtoto cha Minnesota cha Dola 3,222, ambacho kilitajwa katika nyaraka za awali za mahakama.

Katika hatua za awali za kesi hiyo, wajibu wa Edwards ulikuwa tayari umeongezwa zaidi ya kiwango hicho cha msingi. Hati ya hesabu ya mwezi Mei ilionyesha marekebisho ya ziada na jumla ya malipo ya Dola 12,500.

Edwards tayari alikuwa na agizo jingine la matunzo ya mtoto, ambapo mwezi Julai, jaji wa Georgia alimuamuru kulipa dola 3,222 kwa mwezi za matunzo ya mtoto kwa Ayesha Howard kwa ajili ya binti yao. TMZ ilieleza uamuzi huo kuwa ulikuwa ushindi kwa Edwards baada ya jaji kukataa ombi la kutaka alipishwe kiasi kikubwa zaidi.

Ukijumlisha Dola 3,222 na malipo mapya ya Minnesota ya Dola 14,000, jumla ya malipo yake yaliyoainishwa kwenye amri hizo mbili za mahakama ni Dola 17,222 kwa mwezi (zaidi ya Sh44.8 milioni) na kwa mwaka ni Dola 206,664 (takriban Sh537.3 milioni).

Kesi hiyo mpya imeibua taarifa ya kushangaza kuhusu maisha binafsi ya Edwards, ambaye alidai chini ya kiapo kwamba hajawahi kukutana ana kwa ana na Amir. Pia inaelezwa kwamba Edwards hajaomba haki ya kukaa au kutumia muda na mwanawe.