Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico yachapwa nyumbani, yafuzu nusu fainali UEFA

BARCA (1)

USIKU wa Aprili 14, 2026, Atletico Madrid ikiwa nyumbani, imehimili presha kubwa kutoka kwa Barcelona na kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 3-2, licha ya kupoteza mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali kwa mabao 2-1 jijini Madrid.

Baada ya Barca kuwa nyuma kwa mabao 2-0 kutoka mchezo wa kwanza wakipoteza nyumbani, Lamine Yamal alipunguza pengo la jumla mapema dakika ya tano alipopenyeza mpira chini ya kipa wa Atletico, Juan Musso, kufuatia makosa ya kugusa mpira yaliyofanywa na beki wa zamani wa Barcelona, Clement Lenglet.

Dakika 19 baadaye, mzani ukawa sawa baada ya Ferran Torres kuunganisha pasi ya Dani Olmo na kupiga shuti kali la mguu wa kushoto lililoingia kona ya juu ya lango akiipa Barelona bao la pili na kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-2.

BAR 02

Mashabiki wa Atletico walinyamaza kwa takriban dakika saba, kabla ya Marcos Llorente kupenya upande wa kulia na kumpasia Ademola Lookman ndani ya eneo la hatari na kuirejeshea Atletico uongozi wa jumla wa mabao 3-2.

BAR 01

Barcelona ilipaswa kuongoza kwa mabao 3-0 katika mchezo huo dakika tano kabla, lakini Musso alijitanua vizuri kuokoa kichwa cha kujirusha cha Fermin Lopez aliyekuwa hana ulinzi.

Torres alidhani ameifungia Barca bao la tatu dakika 10 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili alipounganisha mpira uliogonga na kuupiga kwa ustadi hadi kona ya juu ya lango, lakini baada ya uchunguzi wa VAR, bao hilo lilikataliwa kwa sababu ya kuotea.

BAR 03

Wageni Barcelona waliendelea kushambulia, lakini kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita, walibaki wachezaji 10 uwanjani baada ya Eric Garcia kumchezea rafu mshambuliaji wa Atletico, Alexander Sorloth, alipokuwa anakimbilia mpira wa kupenyezwa.

Barcelona waliongeza nguvu mbele na kukaribia kufunga kupitia vichwa vya Robert Lewandowski na Ronald Araujo, lakini walishindwa kuandika historia ya moja ya marejeo makubwa zaidi katika Ligi ya Mabingwa.

Atletico sasa watakutana na mshindi kati ya Arsenal au Sporting CP katika hatua ya nusu fainali, wakisaka kufika fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016.