Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Endrick aingia anga za Arsenal

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mbali ya Arsenal, Liverpool pia imewahi kuonyesha nia ya kumsajili staa huyu dirisha la majira ya baridi lakini Madrid ilikataa kuwapa na badala yake ikamtoa kwa mkopo kwenda Lyon.

ARSENAL inaendelea kumfuatilia mshambuliaji chipukizi wa Real Madrid na Brazil, Endrick, 19, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Olympique Lyonnais.

Inaelezwa Arsenal inasubiri jibu kutoka kwa Madrid ikiwa itakuwa tayari kuwauzia fundi huyo au bado wana mipango naye.

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya ndani kutoka Madrid, mabosi wa klabu hiyo wanamchukulia Endrick kama sehemu ya mipango yao ya muda mrefu na hawapo tayari kuona akienda kwenye timu nyigine kubwa Ulaya.

Mbali ya Arsenal, Liverpool pia imewahi kuonyesha nia ya kumsajili staa huyu dirisha la majira ya baridi lakini Madrid ilikataa kuwapa na badala yake ikamtoa kwa mkopo kwenda Lyon.

Mkataba wa Endrick unatarajiwa kumalizika mwaka 2030 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 21 za michuano yote, amefunga mabao saba na kutoa asisti saba.

Ikiwa Madrid itaamua kumuuza, inaelezwa inaweza kuhitaji zaidi ya Pauni 70 milioni kama ada yake ya uhamisho.


Maxi Araujo

ARSENAL imeanza mazungumzo na Sporting CP kuhusu kumsajili winga wa klabu hiyo na Uruguay, Maxi Araujo, 26.

Hata hivyo, Arsenal inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Manchester City na Manchester United ambazo pia zinamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo.

Araujo amevutia vigogo wengi Ulaya kutokana na kasi yake, uwezo wa kucheza pande zote za uwanja na mchango wake katika mashambulizi, jambo linalomfanya kuwa chaguo la klabu nyingi. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Ederson

MANCHESTER United imeongeza jina la kiungo raia wa Brazil, Ederson, 26, anayekipiga katika Atalanta, kwenye orodha yao ya walengwa wa majira ya kiangazi.

Ederson anatajwa kama kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kuanzisha mashambulizi, sifa ambazo zinaendana na mahitaji ya Man United inayotafuta mbadala wa Casemiro.

Baada ya kuonyesha kiwango bora katika Serie A na michuano ya Ulaya, Ederson anadaiwa huenda akauzwa kwa takribani Pauni 70 milioni kiasi ambacho kinaweza kupanda au kushuka kulingana na ushindani wa timu zinazomhitaji.


Tijjani Reijnders

KIUNGO wa Manchester City, Tijjani Reijnders, 27, ameanza kutazama  timu nyingine anazoweza kujiunga nazo Ulaya baada ya kuona mambo yanazidi kwa magumu kwa upande ndani ya kikosi cha matajiri wa Jiji la Manchester.

Reijnders hapati nafasi ya kutosha Man City hali inayosababisha afikirie kuondoka ili kwenda sehemu atakayoonyesha makali yake. Hata hivyo, hadi sasa bado haijajulikana ikiwa Man City itakuwa tayari kumruhusu aondoke mwisho wa msimu.


Abde Ezzalzouli

LIVERPOOL inaripotiwa kuwa tayari kulipa takriban Euro 60 milioni kumsajili winga wa Real Betis na Morocco, Abde Ezzalzouli, 24, dirisha lijalo.

Ezzalzouli ameonyesha kiwango bora sana msimu huu ndani ya La Liga na amefunga mabao 12  katika mechi 38 za michuano yote.

Liverpool inamtazama kama nyongeza muhimu ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu ujao. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Lucas Bergvall

KIUNGO wa Tottenham Hotspur na Sweden, Lucas Bergvall, 20,  ameripotiwa kuwa tayari kukataa ofa kutoka kwa Chelsea  na Aston Villa  zinazohitaji kumsajili katika dirisha lijalo.

Ripoti zinaeleza Bergvall ataendelea kubaki kama Spurs itafanikiwa kusalia Ligi Kuu England msimu ujao. Villa na Chelsea zinafanya harakati za chini chini na zitawasilisha ofa mara tu baada ya kuona Spurs imeshuka daraja.


Conor Gallagher

CONVENTRY City ambayo imepanda daraja kucheza Ligi Kuu England msimu ujao, inaripotiwa kupanga matumizi makubwa ya takriban Pauni 200 milioni kufanya usajili utakaowawezesha kufanya vizuri katika ligi hiyo.

Miongoni mwa mastaa ambao imewaeka katika rada zake ni pamoja na beki wa Aston Villa, Pau Torres pamoja na kiungo wa England, Conor Gallagher anayeichezea Tottenham Hotspur.

Hata hivyo, kuwashawishi wachezaji wa klabu kubwa za EPL kujiunga nao inaweza kuwa changamoto kubwa, hivyo huenda wakasajili mastaa wengi kutoka nje.


Rafael Leao

WINGA wa AC Milan na timu ya taifa ya Ureno, Rafael Leao, 26, anaweza kuondoka katika viunga hivyo dirisha lijalo la majira ya kiangazi, baada ya klabu hiyo kuweka wazi ipo tayari kumuuza iwapo timu inayomhitaji itawasilisha ofa nono.

Ripoti zinaeleza Manchester United  na Barcelona zinaitamani sana huduma ya fundi huyu ambaye anauzwa kwa takribani Euro 60 milioni.

Leao ni mmoja wa wachezaji hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji ya Milan kwa sasa na amefunga mabao 10 katika mechi 27 za michuano yote.