Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jezi ya Haaland yazua jambo Wales

JEZI Pict

Muktasari:

  • Cabango alicheza kwa kiwango bora katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Cardiff City, akifanikiwa kumdhibiti Haaland ambaye alishindwa kupata nafasi kubwa ya kuisumbua ngome ya Wales.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa Wales, Ben Cabango amepata kumbukumbu ya kipekee baada ya kuomba na kupewa jezi ya mshambuliaji wa Norway na Manchester City, Erling Haaland, kufuatia ushindi wa Wales wa mabao 2-1 kwenye Ligi ya Mataifa.

Cabango alicheza kwa kiwango bora katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Cardiff City, akifanikiwa kumdhibiti Haaland ambaye alishindwa kupata nafasi kubwa ya kuisumbua ngome ya Wales.

Baada ya filimbi ya mwisho, beki huyo wa Swansea City alitumia nafasi hiyo kumuomba Haaland jezi yake, ombi ambalo mshambuliaji huyo alilikubali.

JEZ 01

“Nilichukua baada ya mchezo. Alikuwa pale tu, nikajiambia, ‘Kwa nini nisiombe?’ Akanipa jezi yake, lakini hakuchukua yangu,” amesema Cabango.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alirejea katika kikosi cha kwanza baada ya Wales kufungwa mabao 2-0 na Denmark mjini Copenhagen Jumapili iliyopita.

Cabango pia alicheza katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mataifa dhidi ya Ureno mjini Lisbon, ambapo alikabiliana na nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo.

“Ni jambo la kushangaza kucheza dhidi ya Ronaldo na Haaland katika kambi moja. Lakini hapo ndipo unapotaka kuwa na kuendelea kubaki kwa muda mrefu iwezekanavyo.

“Unajifunza mengi unapocheza dhidi ya wachezaji kama hawa. Lazima uwe makini muda wote wa mchezo na huwezi kupoteza umakini hata kwa sekunde moja. Hilo labda linanifanya nitoe kiwango changu bora na imekuwa vizuri,” amesema.

JEZ 02

Wales ilipata ushindi huo kupitia mabao ya Dan James na Neco Williams, baada ya Oscar Bobb kuipatia Norway bao la mapema.

Ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Wales katika mechi saba, huku Cabango akifikisha mechi 18 akiwa na timu hiyo ya taifa.

Beki huyo amesema mchezo huo ulikuwa miongoni mwa viwango vyake bora akiwa na Wales.

“Labda ningesema ulikuwa mchezo wangu bora zaidi nikiwa na Wales. Niliufurahia, ulikuwa mpambano mzuri na mwisho tukatoka na ushindi.

“Nafurahia aina hiyo ya mchezo. Mpira unapokuwa wa kugombaniwa, nitajaribu kuupata kwa asilimia 100 na leo hilo lililipa,” amesema.

Kocha wa Wales, Craig Bellamy, alimpongeza Cabango pamoja na beki mwenzake na nahodha, Ben Davies, kwa namna walivyofanikiwa kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Norway.

“Walikuwa bora sana. Walifanya vizuri kweli. Jambo muhimu tulilozungumza kabla ya mchezo na kulifanyia kazi ni kuwazuia wasikaribie eneo letu la hatari.

“Ni rahisi kusema kuliko kutekeleza, lakini ndiyo maana tuliendelea kusukuma na kufanya kazi kuhakikisha tunawaweka mbali na lango letu kadiri tulivyoweza. Walikuwa bora sana,” amesema Bellamy.