Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yamgeukia Alessandro Bastoni

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Bastoni anatajwa kuwa mchezaji mwenye uzoefu mkubwa licha ya umri wake mdogo, jambo linalomfanya kuwa chaguo bora kwa mradi wa muda mrefu wa klabu hiyo.

MANCHESTER United inajiandaa kutumia nafasi ya Barcelona kusuasua kufikia kiwango cha fedha kinachotakiwa na Inter Milan kwa ajili ya beki wa kati, Alessandro Bastoni, 23, ambaye anatawala kwa sasa soko la usajili Ulaya.

Timu hiyo ya England inaamini hali hiyo inaweza kuipa nafasi nzuri ya kuingia haraka kwenye mazungumzo na kukamilisha dili kabla ya wapinzani wengine kuingilia kati. Bastoni ameendelea kuvutia klabu kubwa Ulaya kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza nyuma na kuanzisha mashambulizi na kwa mujibu wa taarifa kutoka Fichajes, viongozi wa United wanaona ni muhimu kuimarisha safu ya beki msimu ujao, hasa baada ya matatizo ya majeraha na kutoridhishwa na baadhi ya mabeki waliopo kwa sasa.

Bastoni anatajwa kuwa mchezaji mwenye uzoefu mkubwa licha ya umri wake mdogo, jambo linalomfanya kuwa chaguo bora kwa mradi wa muda mrefu wa klabu hiyo.

Iwapo dili hilo litafanikiwa, Bastoni anaweza kuwa moja ya usajili mkubwa wa Man United dirisha lijalo la usajili. Hata hivyo, Inter Milan bado haijaonyesha utayari wa kumwachia kirahisi nyota huyo wa Italia, hasa kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi chao.


David Affengruber

MANCHESTER United inaongoza kuwania saini ya beki wa Elche, David Affengruber, 25, kwa ajili ya usajili wa wachezaji dirisha lijalo.

Affengruber ameibuka kuwa miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa kwa karibu na klabu kadhaa kubwa Ulaya kutokana na kiwango chake kizuri msimu huu na taarifa kutoka Tutto Juve zinaeleza kuwa United wamewapiku Atletico Madrid, AC Milan na Juventus katika harakati za kumpata nyota huyo.


Gabriel Martinelli

WINGA wa Arsenal na Brazil, Gabriel Martinelli anasikilizia mazungumzo kati ya klabu yake na Atletico Madrid kuhusu uwezekano wa kubadilishana na Julian Alvarez anayetakiwa Emirates.

Arsenal inaripotiwa kufuatilia uwezekano wa kufanya biashara ya kubadilishana wachezaji ambayo itampeleka Martinelli Atletico Madrid huku Alvarez akitua Emirates.

Taarifa zinaonyesha timu hiyo ya Hispania iko tayari kusikiliza mpango huo ikiwa watakubaliana.


Hugo Larsson

MANCHESTER City wamewasiliana na kiungo wa Eintracht Frankfurt, Hugo Larsson, kuhusu uwezekano wa usajili wa majira ya kiangazi.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Sweden ameonyesha kiwango bora Ujerumani na sasa anawindwa na klabu a za England zinazotaka kuimarisha safu za kiungo.

Liverpool nao wanatajwa kuwa na nia naye kama sehemu ya maboresho, huku Tottenham Hotspur ikiwa tayari kuvunja rekodi ya usajili kumpata nyota huyo.


Yan Diomande

LIVERPOOL ina matumaini ya kumsajili winga wa RB Leipzig, Yan Diomande, dirisha lijalo la usajili wakati Majogoo hao wakiendelea kutafuta wachezaji vijana wenye kasi na ubunifu ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.

Taarifa zinaeleza iwapo dili la Diomande litakuwa gumu, Liverpool wako tayari kuelekeza nguvu kwa mchezaji mwenzake wa Leipzig, Antonio Nusa ambaye ameonyesha uwezo mkubwa msimu huu.


Gleison Bremer

BEKI wa Juventus, Gleison Bremer anaripotiwa kuwa tayari kuondoka kutokana na kutokuwa na uhakika wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Nyota huyo anaonekana kutaka kujaribu changamoto mpya England huku Liverpool na Manchester United zikitajwa zinamwania.

Bremer anaamini bado ana nafasi ya kucheza katika kiwango cha juu Ulaya, jambo linalomfanya kutafuta timu yenye uhakika wa kushiriki michuano mikubwa.


Cristian Romero

KIUNGO wa Chelsea, Enzo Fernandez anaripotiwa kutumia mazungumzo ya mkataba wake mpya kuishauri kumsajili nyota mwenzake wa Argentina, Cristian Romero, kutoka Tottenham Hotspur.

Enzo anaamini Romero anaweza kuongeza uimara mkubwa katika safu ya beki Chelsea.

Romero amekuwa mmoja wa mabeki bora wa Spurs katika misimu ya karibuni kutokana na uwezo wake.


Edmond Tapsoba

KOCHA mpya wa Chelsea, Xabi Alonso, anataka kuongeza beki mpya kabla ya msimu mpya kuanza.

Chelsea wanafuatilia uwezekano wa staa wa kimataifa wa Burkina Faso, Edmond Tapsoba kufanya kazi tena na Alonso kama walivyokuwa Bayer Leverkusen.

Tapsoba ni mmoja wa mabeki waliovutia zaidi Bundesliga kutokana na uwezo wa kucheza soka la kisasa kuanzia nyuma.