Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vinícius Jr aingia anga za Pep Guardiola

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Man City inadaiwa ipo tayari kulipa hadi Pauni 80 milioni kwa ajili ya kumnunua Vinicius dirisha lijalo.

Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazoiwania saini ya mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Vinícius Junior, 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa, Vinicius ambaye mkataba wake wa sasa na Madrid unatarajiwa kumalizika mwakani, hadi sasa bado hajafanya makubaliano ya kusaini dili jipya huku ikielezwa changamoto kubwa ni masilahi pamoja na mwenendo wa timu.

Man City inadaiwa ipo tayari kulipa hadi Pauni 80 milioni kwa ajili ya kumnunua Vinicius dirisha lijalo.

Hadi sasa hakuna mazungumzo rasmi yaliyoanza kati ya wawakilshi wa Man City na mabosi wa Madrid ingawa hilo linaweza kutokea baada ya msimu huu kumalizika.

Vinicius inadaiwa haridhishwi na hali ya timu ambayo imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika matokeo, hivyo kutua Man City ni jambo linalopewa asilimia nyingi.

Hata hivyo, Madrid haionekani kuwa tayari kumwachia staa huyu hasa ikizingatiwa kutokana na umuhimu wake katika kikosi cha kwanza na bado inaendelea kufanya naye mazungumzo ili kumshawishi asaini mkataba mpya.



Anthony Gordon

BAYERN Munich imefanya mawasiliano na Newcastle United kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wao, Anthony Gordon, 25, dirisha lijalo.

Hata hivyo, inaripotiwa kiasi cha pesa ambacho Bayern imewasilisha kama ofa hakifikii bei ambayo Newcastle imeiweka ili kumuuza nyota huyo.

Gordon ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Newcastle kwa muda sasa kutokana na ubora wake ambao umevutia vigogo wengi Ulaya.


Bradley Barcola

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Bradley Barcola anatarajia kuondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi na klabu kadhaa kubwa Ulaya zikiwamo Arsenal, Liverpool na Barcelona zinamfuatilia.

Barola, 23, ameendelea kuvutia vigogo hao kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu wapili sasa.

Iwapo PSG itaamua kumuuza, Barcola anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wataogharimu pesa nyingi kwa dirisha lijalo.


Joao Palhinha

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi amewaambia mabosi wa klabu hiyo watumie kipengele cha kumnunua moja kwa moja kiungo wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ureno, Joao Palhinha, 30, anayecheza katika kikosi chao kwa mkopo.

Inaelezwa Palhinha ambaye msimu huu amecheza mechi 31 za michuano yote ili kuendelea kubakia Spurs mazima klabu hiyo inatakiwa kulipa takribani Pauni 27 milioni kama ada yake ya uhamisho.


Julian Alvarez

BARCELONA inadaiwa kuwa tayari kulipa Euro 100 milioni kwenda Atletico Madrid kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez, 26.

Hata hivyo, Barcelona inataka kwanza kuona kama Álvarez mwenyewe atakuwa tayari kujiunga nao.

Mshambuliaji huyo ameendelea kuwa mmoja wa nyota muhimu wa Atletico kutokana na uwezo wake wa kufunga na kusaidia timu katika kutengeneza mabao.


Will Osula

KOCHA wa Newcastle United, Eddie Howe, anataka mshambuliaji wa Denmark, Will Osula, 22, aendelee kubaki katika viunga vya St James’ Park msimu ujao.

Osula amekuwa akiwindwa na klabu mbalimbali Ulaya na baadhi ya ripoti zilidai anaweza akaondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyu ambaye ana mkataba unaodumu hadi 2029, msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao saba.


Ross Barkley

KOCHA  wa Coventry City, Frank Lampard amefanya mawasiliano binafsi na kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya  England, Ross Barkley, 32, ili kumshawishi akubali kujiunga nao dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Barkley anatarajiwa kumaliza mkataba Aston Villa mwishoni mwa msimu, hali inayomfanya kuwa chaguo rahisi kwa Converty ambayo imepanda daraja kucheza Ligi Kuu England msimu ujao.


Alex Remiro

REAL Sociedad inapambana kumzuia kipa, Alex Remiro, 31, asiondoke dirisha lijalo na vigogo wengi Ulaya wanataka kumsajili ikiwamo Barcelona.

Barcelona imekuwa ikimfuatilia Remiro kwa muda mrefu na inaamini ikiipata saini yake atasaidia kuboresha na kuongeza ushindani eneo la kipa.

Kwa sasa Sociedad inapambana kuhakikisha inamsainisha mkataba mpya Remiro utakaokuwa na masilahi mapana.