Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alisson Becker sasa anukia Juventus

Muktasari:

  • Alisson anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Liverpool hali inayoweza kuwalazimisha majogoo hao kumuuza kwa sasa badala ya kusubiri aondoke bure mwisho wa wa msimu ujao.

JUVENTUS imemuweka kipa wa Liverpool na Brazil, Alisson Becker, 33,  katika vipaumbele vyao vya usajili wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Alisson anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Liverpool hali inayoweza kuwalazimisha majogoo hao kumuuza kwa sasa badala ya kusubiri aondoke bure mwisho wa wa msimu ujao.

Kipa huyo bado ni miongoni mwa wachezaji tegemo wa Liverpool akiwa na uzoefu wa michuano mbalimbali kiasi cha kuwaaminisha Juventus kwamba ikimpata shida yao katika lango itakuwa imemalizika kabisa.

Inaelezwa Becker mwenyewe hana mpango wa kuendelea kusalia katika kikosi cha Liverpool na ameshamwambia hadi wakala wake kwamba anahitaji kupata changamoto mpya sehemu nyingine baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa ripoti, ikiwa itaamua kumuuza, Liverpool inaweza kudai takribani Pauni 25 milioni.

Tangu kuanza kwa msimu huu Becker amecheza mechi 34 za michuano yote.


Mateus Fernandes

MANCHESTER United inamfuatilia kiungo wa kimataifa wa Ureno, Mateus Fernandes, 21, anayeichezea West Ham United ambayo ipo katika hatari ya kushuka daraja. Inaelezwa Fernandes anaweza kuondoka iwapo West Ham itashuka Ligi Kuu, kwani hataki kucheza Championship msimu ujao. Kiungo huyo machachari kwa sasa mawakala wake wapo katika mazungumzo na Man United ingawa bado hakuna mwafaka wowote uliofikiwa.


Manuel Ugarte

MANCHESTER United ipo tayari kumuuza kiungo wa kimataifa wa Uruguay, Manuel Ugarte, 25, kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara. Tangu Michael Carrick ateuliwe kuwa kocha wa muda Januari, Ugarte ameanza mechi moja ya ligi hali inayoonyesha kupungua kwa nafasi yake kikosini. Man United wanaonekana kuwa tayari kufanya uamuzi kuondoa baadhi ya wachezaji ili kurekebisha kikosi na Ugarte anaweza kuwa miongoni mwa mastaa  watakaoondoka dirisha lijalo.


Jannik Schuster

BRENTFORD inaendelea kufanya mazungumzo ya kumsajili beki raia wa Austria, Jannik Schuster, 19, kutoka Red Bull Salzburg. Inaripotiwa kuwa dili hilo linaweza kufikia Pauni 16 milioni na kwa sasa pande zote mbili bado zipo  kwenye mazungumzo. Mabosi wa Brentford wanataka kufanya haraka kuhakikisha nyota huyo anasajiliwa mapema ili kuepuka ushindani kutoka kwa timu nyingine zilizoanza kuinyemelea huduma yake.


Manuel Akanji

INTER Milan inalazimika kutumia kipengele maalumu kinachoitaka kulipa Euro 15 milioni ili kumsajili beki wa Manchester City na timu ya taifa ya Uswisi, Manuel Akanji, 30, ambaye msimu huu anacheza Inter kwa mkopo. Hatua hiyo imekuja baada ya Inter kubeba ubingwa Serie A, kwani katika mkataba wa makubaliano ya kumsajili Akanji ni kwamba ikiwa itachukua ubingwa italazimika kumsainisha mkataba wa moja kwa moja.

Akanji amekuwa katika kiwango bora tangu atue Inter.


Bradley Barcola

LIVERPOOL na Arsenal ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu England zinazomfuatilia straika wa PSG na Ufaransa, Bradley Barcola, 23. Barcola ambaye ameendelea kuonyesha kiwango bora akiwa PSG, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote. Liverpool na Arsenal zinadaiwa kuwa tayari kutoa takribani Pauni 50 milioni ili kumsajili, lakini kiasi hicho kinaonekana kuwa kidogo kwa PSG ambayo inahitaji zaidi.


Joel Ordonez

CHELSEA inamfuatilia beki wa Club Brugge na Ecuador, Joel Ordonez mwenye umri wa miaka 22, ili  kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ordonez pia aliwahi kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Liverpool iliyokuwa tayari kulipa takribani Pauni 43 milioni dirisha la usajili la Januari. Chelsea imevutiwa naye kutokana na upungufu ambao inao eneo la ulinzi.


Alex Remiro

REAL Sociedad inajaribu kumzuia kipa wa kimataifa wa Hispania, Alex Remiro, 31, asiondoke dirisha lijalo la majira ya kiangazi na vigogo wengi Ulaya wanataka kumsajili ikiwa ni pamoja na Barcelona. Wababe hao wamekuwa wakimfuatilia Remiro kwa muda mrefu na wanaamini wakiipata saini yake atasaidia kuboresha na kuongeza ushindani golini. Kwa sasa Sociedad inapambana kumsainisha mkataba mpya.