Wakala wa Lewandowski atua Italia
Muktasari:
- Lewandowski mwenye umri wa miaka 37, alijiunga na Barca mwaka 2022 akitokea Bayern Munich na tangu wakati huo amefunga mabao 119 katika mechi 191 games, akiisaidia kushinda mataji matatu ya La Liga.
BARCELONA, HISPANIA: BAADA kutangazwa kuwa ataachana na Barcelona mwisho wa msimu, wakala wa staa wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, 37, ameripotiwa kufunga safari hadi Italia kukutana na wawakilishi wa Juventus na AC Milan ili kujadili dili la fundi huyo.
Lewandowski mwenye umri wa miaka 37, alijiunga na Barca mwaka 2022 akitokea Bayern Munich na tangu wakati huo amefunga mabao 119 katika mechi 191 games, akiisaidia kushinda mataji matatu ya La Liga.
Staa huyu ni miongoni mwa washambuliaji bora duniani kwa sasa na klabu nyingi zinataji huduma yake kutokana na uzoefu wake.
Mkataba wa sasa wa Lewandowski unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na inaelezwa moja kati ya sababu zilizochangia Barca kufikia uamuzi wa kutomwongezea ni ili kupata nafasi ya kumsainisha mkataba wa moja kwa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ambaye msimu huu anacheza katika kikosi chao kwa mkopo na kuonyesha kiwango bora.
Mbali ya vigogo hao wa Italia, Lewandowski pia anawindwa na matajiri wa Saudi Arabia ambao wapo tayari kulipa pesa nyingi ili kuhakikisha inaipata saini yake.
Tangu kuanza kwa msimu huu, Lewandowski amecheza mechi 40 za michuano yote, amefunga mabao 18 na kutoa asisti nne za mabao.