Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenda alivyotoa mwanya Isamuhyo, mtego wa Chama, Gueye ukinasa mapema

DABI Pict


ILE Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, imemalizika kwa sare ya mabao 2-2, lakini nyuma ya matokeo hayo, kuna mambo mengi yametokea ndani na nje ya uwanja, huku pia yakitoa taswira kuelekea mechi za kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu Bara.


Itakumbukwa kwenye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo mzunguko wa kwanza, zilitoka uwanjani bila ya kufungana, ukichezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Safari hii pale Meja Jenerali Isamuhyo, Dar imeishia kwa sare ya mabao.


Matokeo hayo yameifanya Yanga kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikifikisha pointi 48, ikiiacha Simba nafasi ya pili na pointi 43, tofauti ikiendelea kubaki ileile tano huku zikisalia mechi kumi kuhitimisha msimu huu.

ISAMU 06

DAKIKA 10 ZA MOTO SIMBA

Simba juzi ilianza mchezo kwa kasi kubwa ambapo ilikuwa na dakika 10 za kwanza za moto ikitengeneza mabao mawili ya haraka yakifungwa na viungo Libase Gueye na Clatous Chama yaliyowashtua Yanga.

Ukiachana na kutikisa nyavu mapema, kitu bora ni namna Simba ilivyotengeneza mabao hayo kwa ufundi wa uwanjani ambapo ukitazama utagundua kwamba Simba ilikuwa bora kuwaweka wachezaji wa Yanga kwenye presha kubwa ambayo iliwalazimisha kufanya makosa na kwenda kutengeneza mabao hayo.

Bao la kwanza la Simba lilitokana na makosa ya beki wa Yanga, Israel Mwenda ambaye wakati anapokea mpira kutoka kwa nahodha Bakari Mwamnyeto, alifanya kosa la kutojua kabla ya kupokea mpira alitakiwa kuupeleka wapi, ndipo Chama akafanya kazi kubwa ya kupeleka presha na kufanikiwa kutibua hesabu zake.

Mwingine alikuwa Gueye ambaye wakati Chama anapokonya mpira alionyesha utulivu kama kawaida yake lakini achana na pasi ya maana ya Mzambia huyo, angalia namna Gueye alivyokuwa na mikimbio bora akimtengenezea chaguo sahihi mwenzake na kwenda kumaliza vizuri.


CHAMA NI YULE YULE

Ukiacha ubora wa Chama alivyofanya kwenye bao la kwanza, angalia pia alivyopiga pasi ya bao la pili akiufungua ukuta wa Yanga lakini ile asisti ya Elie Mpanzu ikwa moto zaidi na Mzambia huyo kwenda kumalizia kwa bao la kubinuka.

ISAMU 01

NZENGELI KAMA MVINYO

Wakati Yanga ikiwa nyuma kwa mabao mawili ikionekana kama siku yao itakuwa mbaya lakini alikuwa Maxi Nzengeli ambaye aliirudisha timu hiyo mchezoni kwa kulazimisha shambulizi hilo na kwenda kupiga krosi ndani ya eneo la hatari la Simba na kuwalazimisha mabeki wa wekundu hao kufanya makosa na hatimaye Duke Abuya na mfungaji Prince Dube kufanya kweli kuirudisha timu mchezoni.

ISAMU 05

DAMARO BADO YANGA

Yanga ilipata shida kubwa kwenye eneo la kiungo cha chini, hapa maneno rahisi kuyatumia ni kwamba katika michezo miwili hii dhidi ya Simba, kiungo Mohammed Damaro bado ameshindwa kuonyesha ule ubora mkubwa kama ambavyo alifanya kwenye mchezo dhidi ya Azam hatua ya nusu fainali ya Kombe la Muungano.

Wakati Simba inajipanga kutengeneza bao la pili, Damaro ameonekana akikimbia taratibu akiangalia namna Mpanzu na Chama wakipiga hesabu ya kuufungua ukuta wa Yanga na mpaka wanafanikiwa hakukuwa na na jaribio la kuwasaidia mabeki wa kati kutegua mtego huo wa Simba.

ISAMU 02

YAO AMERUDI

Yanga wakati inarejea kipindi cha pili, ilirudi na mabadiliko mawili akiingia mshambuliaji Laurindo Aurelio ‘Depu’ na Yao Kouassi lakini ingizo la beki huyo raia wa Ivory Coast akichukua nafasi ya Mwenda ndio ilikuwa mwiba mkali kwa Simba.

Yao amerudi ambapo alichofanya ni kuzima nguvu kubwa ya Simba upande wa kulia lakini akawa na kasi ya kupandisha mashambulizi kwenda mbele, tazama namna pasi yake bora ilivyomfuata Depu walioingia pamoja na shuti lake kali likaenda kutengeneza kona ambayo ilitengeneza nafasi ya bao la pili.

ISAMU 04

WAAMUZI WALIZINGUA

Mchezo huo ulisimamiwa na waamuzi kutoka Morocco ambapo mwamuzi wa kati akiwa Hamza El Fareq, msaidizi wake wa kwanza Lahsen Agaou na yule wa pili akiwa Hamza Massiri huku mwamuzi wa nne wa mezani ni Mustapha Kechaf walifanya kazi nzuri lakini bado kuliibuka changamoto mbalimbali katika maamuzi yao.

Fareq alikuwa bora kuwahi kwenye matukio ya mchezo huo lakini aliwanyima Yanga nafasi ya mkwaju wa penalti wakati beki Ismael Toure alipotumia ‘konga’ kumzuia Depu kwenda kufunga.

Naye Massiri aliwanyima Yanga nafasi dakika ya 37 akidai Pacome Zouzoua alikuwa ameotea wakati akipokea pasi ya Allan Okello akiipotezea timu mgeni nafasi nzuri ya kwenda kutengeneza bao.

Kosa lingine la El Fareq lilionekana dakika ya 63 alipotoa kadi kwa kocha Pedro Goncalves wa Yanga badala ya meneja wa timu hiyo Walter Harrison alipotofautiana na Chama.

ISAMU 03

UWANJA MH!

Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliotumika kwa mechi hiyo haukuwa mzuri kwa kiwango cha dabi ambapo eneo la kuchezea lilionekana kuathiriwa na maji na kama utahitajika kutumiwa kwenye mechi kubwa kama hiyo unatakiwa kuwa vizuri kwani ulizilazimisha timu zote kucheza mipira mirefu.


SIMBA PASI BALAA

Simba ilikuwa ndio timu iliyopiga pasi nyingi kwenye mchezo huo ambapo ilimaliza dakika 90 ikiwa imepiga jumla ya pasi 247, kati ya hizo zilizofika 245, zilizopotea 45.

Yanga ilipiga jumla ya pasi 222, zilizofika 191, wakati zile zilipotea 31, huku timu hizo zikigawana vipindi katika kucheza vizuri.