Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paul Peter ajibebeshe deni Taifa Stars

MEXIME Pict

Muktasari:

  • Haikutegemewa baadhi ya wachezaji kuachwa katika kikosi hicho kutokana na viwango bora ambavyo wamekuwa wakivionyesha siku za hivi karibuni huku baadhi ambao hawaonekani wako vizuri wakichukuliwa.

UTEUZI wa wachezaji 28 watakaoipeperusha Bendera ya Tanzania katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baadaye mwezi huu umezua mjadala kidogo.

Haikutegemewa baadhi ya wachezaji kuachwa katika kikosi hicho kutokana na viwango bora ambavyo wamekuwa wakivionyesha siku za hivi karibuni huku baadhi ambao hawaonekani wako vizuri wakichukuliwa.

Mfano wa wachezaji ambao wengi tuliamini atapanda ndege na kwenda Morocco kwenye AFCON 2025 ni mshambuliaji wa JKT Tanzania, Paul Peter ambaye amekuwa tishio kwa nyavu za wapinzani msimu huu.

Peter mwenye umri wa miaka 26, kwa sasa ndiye kinara wa chati ya ufungaji bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa ameshafunga mabao matano kwenye mechi 10 alizowatumikia Maafande hao.

Hata hivyo, Paul Peter hapaswi kuutazama uamuzi huo wa benchi la ufundi la Taifa Stars kumuacha kwa hisia hasi, bali alione kama jambo chanya kwa upande wake ili liwe chachu kubwa kwake kufanya vizuri zaidi siku za usoni.

Ajione ana deni la kuthibitisha uwezo wake kwa kuwa na mwendelezo mzuri wa kile anachokifanya sasa ili kulishawishi benchi la ufundi kuamini anachokifanya siyo cha kubahatisha bali ni uwezo wake.

Umri alionao bado unampa fursa ya kucheza Fainali nne tofauti za AFCON zijazo kwa vile mashindano hayo yanachezwa kila baada ya muda wa miaka miwili hivyo akicheza fainali za mwaka 2033 atakuwa na umri wa miaka 34.

Ikumbukwe nyota wawili wa safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars, Mbwana Samatta na Saimon Msuva umri umeanza kuwatupa mkono, hivyo muda siyo mrefu wanaweza kutangaza kutundika madaruga.

Uwanja utakuwa mkubwa kwa Paul Peter na washambuliaji wenzake ambao hawajaitwa hivi sasa, hivyo kijiwe tunawaomba wasiwe na presha.