Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakosoaji, washauri mradi wa Uwanja Yanga wasikilizwe

ZENGWE Pict


Kuna tabia ambayo ilikuwepo zamani na ilikuwa inatumiwa na wanachama wa klabu za Simba na Yanga, maarufu kama ‘makomandoo’ ya kumtukana na kumzonga mwanachama au mtu yeyote anayejitokeza kukosoa jambo linalofanywa na viongozi, hasa wa juu.


Tabia hiyo ilichelewesha sana maendeleo na ilitumiwa na viongozi wajanja kutangaza ahadi hewa kwa wanachama na kutumia ahadi hiyo kujiweka madarakani kwa muda mrefu wakijua yeyote atakayehoji ahadi yake atashambuliwa kwa matusi na maneno mengine ya fedheha.


Kwa hiyo mambo yalikuwa hayaendi lakini kiongozi analindwa kwa nguvu kubwa kwa sababu uwepo wake madarakani ulinufaisha hao makomandoo.

ZENG 01

Kwa hiyo, utamaduni wa kuhoji au kukosoa kwenye mikutano mikuu ya klabu hizo ukatoweka na ikabidi wakosoaji au watoaji maoni tofauti na ya yule kiongozi, wafanye hivyo kwa mbali sana; kwa kuitisha mikutano na waandishi wa habari na kutoa ya rohoni.

Tabia hii inarudi kwa kasi sana na kibaya zaidi, utukanaji sasa unaenda hadi kwa wachezaji wanapofanya makosa uwanjani.

Na kwa sababu mawasiliano yamerahisishwa na teknolojia, ni rahisi kwa shabiki au mwanachama kumshambulia kwa matusi mchezaji na lengo lake likafanikiwa, yaani mchezaji akaupata ujumbe mapema sana. Ilikuwa hivyo kwa Isra Mwenda wa Yanga baada ya kufanya kosa lililozaa bao la kwanza wakati wa mechi ya fainalin ya Kombe la CRDB. Isra alipokonywa mpira wakati Yanga wakianza kupanga shambulizi na kusababisha bao hilo la kwanza.

ZENG 02

Habari zinasema beki huyo wa kulia aliyefanya kazi kubwa wakati Yao Kouasi akiwa majeruhi, ameomba kupumzika ili atulize akili baada ya kupokea rundo la matusi kutoka kwa mashabiki na wanachama.

Imekuwa hivyo tena kwa nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye klabu hiyo imesema ameomba atulize akili kwa muda baada ya kushambuliwa yeye na familia yake kwa matusi kutokana na makossa mawili aliyofanya katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji.

Ni Mwamnyeto ambaye ameishika ngome ya Yanga kwa muda mrefu tangu Dickson Job aumie wakati wa mechi ya kwanza dhidi ya Simba mapema mwaka huu. Mwamnyeto pia amekuwa nguzo muhimu ya Yanga katika mechi muhimu ambazo alikosekana mmoja wa mabeki tegemeo wa kati, yaani Job na Ibrahim Bacca.

ZENG 03

Cha kushangaza ni jinsi mashabiki walivyosahau hayo yote, likiwemo bao la kusawazisha la Yanga katika mechi dhidi ya Simba iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2 mapema mwezi huu, kiasi cha kumrushia matusi yaliyosababisha aone hana thamani na kuomba kupumzika kwa muda.

Lakini Kouasi ambaye alijiuza kirahisi katika shambulizi la kushtukiza la Dodoma Jiji na kumpa urahisi Waziri Mahadhi kufunga bao la pili kirahisi, hajashambuliwa kwa maneno yoyote mabaya, achilia mbali matusi.

Hata Prince Dube ambaye alipoteza nafasi nyingi za wazi siku ya mechi ya Dodoma Jiji na hata nafasi ya dhahabu ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Simba, hajashambuliwa kwa matusi kama ambavyo mzawa Mwamnyeto na Isra wamekumbana na moto huo.

Hii ni tabia mbaya kwa mashabiki kuchukulia kosa moja ndiyo mwisho wa dunia.

Mbali na kutukana wachezaji wanaofanya makossa, wanachama na mashabiki hawa sasa wanatukana yeyote anayejaribu kutoa maoni tofauti kuhusu mradi wa kujenga uwanja maeneo ya Jangwani.

ZENG 04

Ni kama wanaona uongozi umefanya kila kitu kwa usahihi na hivyo hakuna haja ya kujishughulisha kuzungumzia maoni au ukosoaji unaofanywa na mashabiki na wanachama.

Maelezo yanayotolewa kuhusu mkataba na mpango wa ujenzi wa uwanja huo wa kisasa, bado hayajatosheleza wadau kujua jinsi hali itakavyokuwa. Bado kuna ukakasi m wingi kuhusu mkataba na GSM, ni kwa nini klabu imeingia na kampuni hiyo isiyo na shughuli za ukandarasi au labda inafanya shughuli hizo.

Tunajua viwanja kama Emirates wa Arsenal, ambao ulibajetiwa utumie Pauni milioni 390 za Kiingereza ulianza kujengwa kwa mkopo wa Pauni milioni 260 kutoka benki, kabla ya suala hilo kuhamishiwa kwenye bondi, kampuni ya usafiri wa anga ya Emirates kuweka Pauni milioni 102 kwa ajili ya haki za jina, mauzo ya ardhi ya ziada  na mauzo ya Uwanja wa Highbury.

Kwa hiyo, ukiangalia hayo unaona fedha zinatoka wapi na kwa ukubwa wa mradi unaona jinsi ambavyo klabu itaweza kurejesha mkopo ambao ulisababisha Kocha Arsene Wenger awe na bajeti ndogo ya usajili hadi deni lilipoisha ndio akasajili wachezaji ghali, akianzia na Ozil.

Uwanja wa Allianz Arena ulijengwa kwa mkopo wa Euro milioni 346 uliochukuliwa na kampuni ya Munchen Stadion iliyokuwa inamilikiwa na klabu za Bayern Munich na TSV 1860 Munich. Lakini mwaka 2006 Bayern ikanunua hisa zote za TSV na kuwa mmiliki wa kampuni hiyo kwa asilimia 100.

ZENG 05

Mkopo ulikuwa ulipwe mwaka 2030, lakini Bayernm ikaumaliza mwaka 2014 huku kampuni ya bima ya Allianz ikinunua haki za kutumia jina la uwanja.

Jiji la Munich na jimbo la Bavaria zilichangia Euro 210 kwa ajili ya uendelezaji wa eneo linalozunguka uwanja huo, yaani kupanua barabara na stesheni ya treni iliyo jirani.

Kwa hiyo, ukiangalia maelezo hayo unaona kunakosekana habari nyingi kuhusu mpango huo ambazo ninahisi zipo lakini hazijatolewa kwa wadau na ndiyo maana wanahoji.

Makisio ya gharama za uwanja si kitu kinachozungumzwa kama jambo muhimu, bali umiliki. Kila kunapokuwa na mpango wa ujenzi wa uwanja, gharama zake huwa ni muhimu. Ndiyo maana leo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anahoji tofauti kubwa iliyopo katika makisio na gharama za Uwanja wa Samia Suluhu unaojenga mkoani Arusha.

Hata Rais Benjamin Mkapa alipoanza mpango wa kujenga uwanja, makisio ya awali ya gharama yalikuwa ni Sh54 bilioni ingawa ujenzi ulichukua fedha nyingi zaidi.

Kujua makisio pia huwezesha kujua fedha hizo zitatoka wapi na Rais Mkapa alisema zitatokana na kodi za wananchi, wakati zile za Uwanja wa Samia zilipitishwa na wabunge.

Kwa hiyo, kuna mambo muhimu ambayo wadau wanahoji na ni muhimu yajibiwe sasa ili kuepusha suala hilo kuonekana linapelekwapelekwa kwa kuwa kuna wanachama na mashabiki hawaelewi kitu na wanaoelewa wanaogo[pa kutukanwa na kundi dogo linaloulinda uongozi.

Ni muhimu kuacha kushambulia wanaokosoa kwa kuwa wanasaidia kuona tatizo. Hata kama wanachosema si sahihi, ukosoaji wao humaanisha kuna jambo linatakiwa liwekwe sawa ili umma uelewe zaidi.