Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga na kitendawili cha shibe inayozalisha njaa

ZENGWE Pict


Pengine Yanga wanataka waanze msimu mpya wakiwa wapya kabisa baada ya kumtimua Kocha Concalves Pedro kwa kile walichoeleza hakuwa na kiwango kizuri licha ya timu kuendelea kuongoza Ligi Kuu tangu aichukue Oktoba 25 mwaka jana.


Kutimuliwa kwa Mreno huyo kulikuja baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 na Simba katika fainali ya mashindano ya Kombe la Muungano, baadaye kutoka sare ya mabao 2-2 na Simba kabla ya kuishinda kwa taabu KMC wakati Allan Okello alipofunga bao pekee. Pedro hajawahi kuwa na wakati mzuri Yanga. Akishinda kwa bao 1-0, analalamikiwa timu imeshuka kiwango.


Alipotua tu nchini, mijadala ilianza, Yanga imefanya makosa kwa kumwajiri kocha ambaye hajawahi kufundisha katika ngazi ya klabu kwa kuwa muda mwingi amekuwa kwenye timu za taifa za vijana.

ZENG 01

Pedro akipata ushindi mkubwa, hasifiwi na badala yake kunaibuka tuhuma Yanga inanunua mechi. Na akipata ushindi wa kawaida wa mabao 2-0 au 3-0, mijadala huhamia kwenye matukio yanayokuja kutafsiriwa wapinzani walionewa kwa kunyimwa ama penati au kupuliziwa filimbi ya kuotea.

Kwenye vyombo vya habari, mijadala imekuwa ni kushuka kiwango cha timu. Hakuna vigezo vinavyotumiwa kuonyesha kiwango cha timu kimeshuka, lakini mijadala huwa mikubwa tu kana kwamba timu inatakiwa iwe inashinda kwa mabao kuanzia manne kwenda juu.

Kwa takwimu, hakuna ambaye amewahi kuweka mezani taarifa zake kuonyesha kushuka kwa kiwango kwa kuwa hata timu ya Nasredine Nabi kuna wakati ilikuwa inashinda kwa bao 1-0 na hata ile ya Miguel Gamondi ilipitia kipindi hicho.

ZENG 02

Bahati mbaya sana, inaonekana kama viongozi wa Yanga nao wameingia kwenye mkumbo huo. Taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari wakati akiongea na kituo kimoja cha redio inasema pamoja na takwimu kuwa nzuri, Yanga haiangalii takwimu bali “performance” au labda mchezo.

Performance inapimwa na nini hasa? Kama ni takwimu, kipimo cha kisayansi kabisa, Pedro alikuwa mzuri. Tangu aanze kuifundisha Yanga hajawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi katika mechi 19, akiwa amefunga mabao 44 na kuruhusu matano tu na hadi sasa amekusanya pointi 51.

ZENG 03

Takwimu za uwanjani zinaonyesha timu yake ndio inatawala mchezo karibu katika mechi zote na kutikisa nyavu hata katika mechi ambazo wapinzani waliamua kupaki basi golini, kama ilivyokuwa katika mechi dhidi ya KMC, ambayo Yanga ilicheza kwenye robo ya wapinzani kwa muda mwingi.

Kwa hiyo, unaweza kujiuliza hicho kiwango kinachozungumziwa na Yanga kinajumuisha mambo gani? Au ni hofu?

ZENG 04

Kamwe anasema hawataki kuanza kustuka wakati timu imeshapoteza mechi ndiyo maana wameamua kuchukua uamuzi mapema. Hata Bayern Munich, ambayo kwa misimu miwili imekuwa ya moto, hupoteza mechi bila ya kiwango kushuka kama ilivyokuwa wiki iliyopita ilipoondolewa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Hofu ya Yanga imeegemea wapi?

Pengine viongozi wa Yanga hawajui wanataka nini au imekuwa ni kawaida kutimua kocha baada ya kipindi fulani ili wajipe kazi ya kutafuta mwingine?

ZENG 05

Kwa kawaida kuna makocha wa aina mbili; wale wa kiufundi (techinicians) na wale wa mbinu (tacticians). Makocha wa kiufundi ni wale wanaowapa wachezaji mambo muhimu ya kiufundi na kutegemea zaidi kuelewana kwao nje na ndani ya uwanja ili timu iwe imara. Makocha kama Carlo Ancelotti na Zinedine Zidane hutegemea sana maelewano ya wachezaji kujenga timu imara.

Wale wa mbinu hutegemea sana kuwapa wachezaji majukumu uwanjani na hupanga wale wenye nidhamu na mbinu zake. Hawa unaweza kuwaambia unataka ushindi na wakakupa bila yaw ewe kufurahia. Hawa hawajali timu inacheza vizuri kiasi gani wala vibaya, wanachojali ni matokeo ya mwisho.

Wale wa ufundi huhitaji muda mrefu kujewnga timu imara wakati wale wa mbinu huhitaji muda mfupi kwa kuwa anapanga mchezaji anayefuata kikamilifu maelekezo yake an kosa moja la kizembe linaweza kumpoteza mchezaji.

ZENG 06

Yanga wanahitaji kocha mwenye falsafa gani ili waweze kukaa naye muda mrefu? Ikiwa wanahitaji kocha wa mbinu, wako tayari kupokea matokeo bila ya mchezo mzuri? Kama wanahitaji wa ufundi, wako tayari kusubiri muda mrefu?

Nabi, ambaye anasifika kwa kujenga timu inayoendelea kutembelea makali yake, alifundisha Yanga kwa misimu miwili, kuanzia Aprili 2021 hadi Jumi 2023, na kufuatiwa na Gamondi aliyeanzia Julai 2023 hadi Novemba 2024.

Kuanzia hapo Yanga ilianza timuatimua. Akaajiriwa Saed Ramovic (Novemba 2024 hadi Februari 2025) na kufuatiwa na Miloud Hamdi (Februari 2025 hadi Julai 2025). Baadaye akaajiriwa Roman Folz (Julai 2025 hadi Oktoba 2025) na ndipo alipotua Pedro.

Kwa kifupi unaona makocha waliosifika sana ni wale waliodumu muda mrefu kutokana na kuelewa vizuri soka la Tanzania na mazingira yake pamoja na wachezaji wake na hivyo kusuka mikakati imara.

Inaonekana viongozi wa Yanga huenda sokono kusaka makocha bila ya kujua wanahitaji kocha wa aina gani kulingana na kikosi walichonacho au wanataka nini na hivyo kujua wanahitaji nini kutoka kwa kocha huyo.

Kama wanachohitaji ni ushindi, wawe tayari kufurahia matokeo bila ya kujali yamepatikanaje. Kama wanataka kujenga kikosi imara kitakachofanya vizuri kwa muda mrefu, basi wawe na subira, lakini si ile ya kukubali vipigo bali kujua mwenendo wa kukua kwa timu ambao utawapa matumaini ya nini wanataka.

Lakini ni muhimu kwao kujua kuwa nao wanachangia kwa timu kufanya vizuri au kufanya vibaya. Kama kocha ameletewa wachezaji watano wapya, halafu wote hawawezi kuingia kikosi cha kwanza na wanaachwa dirisha dogo, ni lazima mipango ya kocha itavurugika.

Pia kama viongozi wako tayari kusema Jammeh alikuwa ni chaguo la Pedro, wawe tayari kusema wengine walioboronga ni chaguo la nani!