Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba anzeni upya, utulivu unahitajika

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Msimu huu, kwa uhalisia wake, unapaswa kuhesabiwa kuwa wameshafunga pazia, hususan katika mashindano ya kimataifa ambapo Simba haikufikia matarajio ya wanachama, mashabiki na wadau.

HUU ni wakati sasa kwa Klabu ya Simba kufanya tathimini ya kina na kuanza upya kwa umakini mkubwa kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Msimu huu, kwa uhalisia wake, unapaswa kuhesabiwa kuwa wameshafunga pazia, hususan katika mashindano ya kimataifa ambapo Simba haikufikia matarajio ya wanachama, mashabiki na wadau.

Tunapozungumzia Ligi ya Mabingwa Afrika, ni wazi kuwa Simba ilikosa uthabiti wa kiufundi, kimbinu na kiuongozi unaohitajika kushindana katika kiwango cha juu na kwa hakika kwa sasa ni kama inapiga hesabu za TUKIWAKI.

PUMZ 01

Kwa miaka mingi Simba ilizoweleka kufanya maajabu katika mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), yaani Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho ambako imetinga robo fainali mara saba katika miaka ya karibuni.

Hatua ya kwanza ni kuwa na utulivu wa ndani. Simba haina budi kukaa chini kwa utulivu mkubwa, bila jazba wala lawama na kufanya tathimini ya kweli kujua ni wapi hasa mambo yalikwenda kombo.

Ukweli mchungu ni kwamba anguko la Simba halijaanza leo wala jana; lilianza kitambo. Kwa misimu ya karibuni, klabu hiyo imekuwa ikiyumba katika maeneo mengi, lakini zaidi katika sera ya usajili wa wachezaji.

PUMZ 02

Kumekuwa na mtindo wa kusajili wachezaji wengi kila dirisha la usajili, kisha kuwaacha wengi wao baada ya miezi sita kabla hata timu haijapata muunganiko wa uhakika wa kiuchezaji kweli.

Matokeo yake ni timu isiyo na utambulisho, mwendelezo na isiyowapa wachezaji mazingira ya kujiamini na kung’ara. Kinachozua maswali zaidi ni pale wachezaji haohao wanaoachwa Simba wanapojiunga na timu zingine na kuonyesha viwango bora jambo linaloashiria kuwa tatizo halikuwa uwezo wao pekee, bali mazingira, mifumo na pengine uamuzi wa kiuendeshaji ndani ya klabu.

Simba inahitaji kuja na ufumbuzi wa uhakika wa matatizo yake, siyo ufumbuzi wa kupapasa au kuoneana aibu. Kimsingi uongozi wenyewe unapaswa kujitathmini upya kwa ujasiri, je, bado unafaa kuiongoza taasisi hiyo kubwa katika mazingira ya ushindani mkubwa wa soka la kisasa? 

PUMZ 03

Simba siyo timu ndogo; ni taasisi yenye historia, mamilioni ya mashabiki na matarajio makubwa. Taasisi ya aina hiyo inahitaji viongozi wanaoweza kufanya uamuzi kwa wakati, weledi na maslahi mapana ya klabu siyo kusuasua au ubabaishaji.

Katika mazingira ya sasa ya soka, uongozi hauhitaji tena ubabaishaji, bali misimamo thabiti ya kiuongozi, mipango ya muda mfupi na mrefu, na utendaji unaopimika kwa matokeo. Siyo ajabu wala aibu kuanza upya.

Kinyume chake, ni ishara ya busara kukubali pale ulipokosea na kuchukua hatua sahihi. Hata hivyo, Simba ikumbuke jambo moja muhimu - wanachama na mashabiki wanataka kuona matokeo uwanjani.

PUMZ 04

Hicho ndicho kipimo kikuu cha mafanikio na siyo kauli wala mipango mizuri kwenye makaratasi. Mwisho, Simba inapolenga kuingia kwenye mfumo wa hisa ni lazima ikumbuke kwamba uwazi siyo jambo la hiari, bali ni wajibu.

Michakato yote ya ndani na nje kuanzia masuala ya kifedha, usajili hadi uendeshaji wa klabu ni lazima viwe wazi, vya kuaminika na vinavyojengwa juu ya misingi ya uwajibikaji. Hapo ndipo Simba itaweza kujijenga upya, kurejesha imani ya mashabiki na kurejea kwa nguvu katika ushindani wa ndani na kimataifa.