Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker ainyooshea kidole Yanga, aipa tahadhari

BACKER Pict


KOCHA Mkuu wa Simba, Steven Barker, amesema ushindani wa Ligi Kuu Bara msimu huu umekuwa mkubwa, lakini anaamini kikosi chake kipo tayari kuendelea kupambana na kuiwekea presha Yanga katika mbio za ubingwa.


Barker amesema kuna mechi kadhaa zimekuwa ngumu kwa Simba hadi sasa, lakini wachezaji wake wamekuwa wakipata nguvu ya ziada kutokana na mambo mawili muhimu yanayowasukuma kupambana hadi dakika ya mwisho kutafuta ushindi.


Kocha huyo amesema jambo la kwanza ni kiu kubwa ya klabu kutaka kurejesha taji la Ligi Kuu Bara, huku la pili likiwa ni kutotaka kuwaangusha mashabiki ambao wameonyesha imani kubwa kwa timu hiyo msimu mzima.

BARKER Pict

“Ni kweli tumekuwa na mechi ngumu katika kipindi hiki, lakini wachezaji wanafahamu kilichopo mbele yetu. Kila mmoja anatambua umuhimu wa kupigania ubingwa na wakati huohuo hatutaki kuwavunja moyo mashabiki wetu ambao wamekuwa nyuma yetu muda wote nafikiri kila mmoja ameona jinsi ambavyo tumekuwa tukipambana,” amesema Barker.

Barker alifichua ndani ya klabu hiyo suala la ubingwa limepewa uzito mkubwa kiasi kwamba kila kiongozi anayekutana na wachezaji amekuwa akisisitiza umuhimu wa kutwaa taji hilo mwishoni mwa msimu.

BARKER Pict

“Hakuna kiongozi ambaye amewahi kuzungumza na timu bila kusisitiza umuhimu wa kushinda ubingwa msimu huu. Hilo limekuwa jambo linalorudiwa mara kwa mara na kila mtu ndani ya klabu anatambua wajibu wake,”  amesema.

Kocha huyo ameongeza sapoti kutoka kwa mashabiki imekuwa silaha nyingine muhimu inayowapa morali ya kupambana kwa nguvu zaidi kila wanapoingia uwanjani.

BARKER Pict

“Ukiangalia kila tunapocheza, iwe nyumbani au ugenini, utaona namna mashabiki wanavyojitokeza kwa wingi. Wanaonyesha wazi wana kiu ya kuona Simba ikitwaa ubingwa msimu huu na hilo linatupa motisha kubwa sana,” amesema Barker.

Simba imeendelea kuwa kwenye mbio za kuwania ubingwa msimu huu ikiwa imekosa ubingwa huo kwa misimu minne mfululizo baada ya kuzidiwa kete na wapinzani wao wakubwa Yanga.

BARKER Pict

Ikumbukwe Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 60 katika mechi 25 ilizocheza, huku Simba ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 58.

Timu zote zimepoteza mechi moja kila moja msimu huu na kunaonekana kuwa na ushindano mkubwa zaidi kwenye michezo mitano iliyobaki ili ligi imalizike.