Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraza aiandalia mkakati Singida Black Stars

BARAZA Pict

Muktasari:

  • Singida Black Stars katika mechi sita za mashindano msimu huu imeshinda tano na sare moja ikifunga mabao tisa na kuruhusu mara tatu.

KOCHA Mkuu wa Pamba Jiji, Francis Baraza amesema wana kazi kubwa ya kufanya kukabiliana na Singida Black Stars ambayo ameitaja kuwa ni timu tishio kutokana na kutofungwa mechi yoyote msimu huu.

Singida Black Stars ambayo imefuzu kushiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, kwenye mechi sita za mashindano yote ilizocheza, mbili Ligi Kuu Bara na nne Kombe la Shirikisho Afrika, haijapoteza hata moja. Itakutana na Pamba Jiji Novemba 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Baraza amesema wana faida ya kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini wana kazi kubwa ya kufanya kujiandaa kimbinu kuikabili Singida Black Stars kutokana na rekodi nzuri waliyonayo wapinzani wao.

“Ukiondoa rekodi hiyo pia wana timu imara iliyo na wachezaji wengi wazoefu, kazi niliyonayo ni kuwaandaa wachezaji wangu kwa kuhakikisha wanakuwa timamu kuikabili timu hiyo kwa dakika 90 na kusuka mipango imara maeneo yote.

“Tunaenda kukutana na timu bora kwenye maeneo mengi na sisi pia ni bora, ila kazi kubwa itafanyika ili kuidhibiti Singida kwa kuwa timu ya kwanza kuifunga, haitakuwa rahisi lakini hilo linawezekana,” amesema.

Baraza amesema anafurahia kurudi kwa wachezaji wake wengi ambao walikuwa majeruhi, anaamini kumeongeza chachu ya kuwa na kikosi kamili ambacho kitampa machaguo sahihi kuikabili Singida Black Stars.

“Tulikuwa na wakati mgumu kwenye mechi za mwanzo wa msimu kutokana na kuwakosa baadhi ya wachezaji hasa eneo la ushambuliaji kwani wengi walikuwa majeruhi, sasa wamerejea na wanaendelea vizuri na maandalizi,” amesema. Katika Ligi Kuu Bara msimu huu, Pamba Jiji imecheza mechi nne, imeshinda moja, sare mbili na kupoteza moja, imekusanya pointi tano na kukamata nafasi ya 10 kwenye msimamo kabla ya mechi ya jana.

Singida Black Stars katika mechi sita za mashindano msimu huu imeshinda tano na sare moja ikifunga mabao tisa na kuruhusu mara tatu.