Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcola, Mbaye ni suala la muda tu Liverpool

BARCOLA Pict

Muktasari:

  • Barcola, mwenye umri wa miaka 23, amekuwa kwenye orodha ya muda mrefu ya wachezaji wanaotamaniwa na Liverpool, lakini mpango wa kumsajili bado haujakamilika.

LONDON, ENGLAND: WACHEZAJI wanaowindwa na Liverpool, Bradley Barcola na Ibrahim Mbaye, wameendelea kuachwa nje ya kikosi cha Paris Saint-Germain (PSG), hali inayozidisha sintofahamu kuhusu hatma yao katika klabu hiyo.

Barcola, mwenye umri wa miaka 23, amekuwa kwenye orodha ya muda mrefu ya wachezaji wanaotamaniwa na Liverpool, lakini mpango wa kumsajili bado haujakamilika.

Mbaye, mwenye miaka 18, naye anaonekana kuwa chaguo jingine linaloweza kuzingatiwa na Liverpool katika harakati za kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

BARCO 01

Hata hivyo, wawili hao hawajashiriki katika mchezo wa pili mfululizo zilizopita baada ya kuachwa na kocha Luis Enrique.

Kwa mujibu wa taarifa za Fabrizio Romano, Barcola na Mbaye hawatajumuishwa katika kikosi cha PSG kilichocheza dhidi ya Rennes jana Jumapili katika mchezo wa kwanza wa msimu mpya wa Ligue 1.

BARCO 02

Wawili hao pia hawakuwepo katika kikosi kilichopoteza fainali ya Trophee des Champions dhidi ya Lens wiki iliyopita.

Hali hiyo imekuja baada ya kutoshiriki pia katika ushindi wa PSG dhidi ya Aston Villa kwenye UEFA Super Cup siku chache kabla ya mchezo huo.

Barcola na Mbaye walishiriki Kombe la Dunia wakiwa na Ufaransa na Senegal, mtawalia, lakini kwa sasa wanakabiliwa na ushindani mkubwa wa nafasi katika kikosi cha Enrique.

BARCO 03

Ousmane Dembele, Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia tayari ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi hicho, huku PSG ikiongeza ushindani kwa kumsajili Maghnes Akliouche kutoka Monaco.

Enrique alikosolewa baada ya uamuzi wake wa kuwaacha Barcola na Mbaye nyumbani kabla ya mchezo dhidi ya Lens, huku kocha huyo akiondoka kwenye mahojiano ya baada ya mchezo kwa hasira.

Katika mkutano na waandishi wa habari baadaye,Enrique amesema “sisi ni timu changa sana na yenye matarajio makubwa.

“Ni muhimu zaidi kufanya mabadiliko na kutafuta wachezaji wanaofurahia kucheza kwa mtindo wetu na wanaofurahia kuwa PSG.

BARCO 04

“Kama mchezaji hataki kuja, au hafurahii kuwa hapa, ni bora kutafuta suluhisho jingine.”

Barcola pia amewahi kuhusishwa na Arsenal, lakini klabu hiyo ilielekeza nguvu zake kwa mshambuliaji Vinicius Jr kabla ya kushindwa kumnasa.

Barcola anatajwa kuwa na thamani ya pauni140 milioni, kiasi ambacho hadi sasa kimeonekana kuwa kikubwa mno kwa Liverpool.

Kocha wa Liverpool, Andoni Iraola, pamoja na viongozi wa klabu hiyo, wanatarajiwa kuendelea kusaka winga mpya katika siku za mwisho za dirisha la usajili.

Liverpool tayari imewasilisha ofa mbili za kumsajili winga wa Brighton, Jankuba Minteh, lakini zote zimekataliwa licha ya mchezaji huyo kuwa nje kwa sasa kutokana na majeraha.