Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benin yaichapa Botswana, yazoa pointi muhimu

BENIN Pict

Muktasari:

  • Kipa wa Botswana alifanya sevu tatu, dhidi ya moja ya kipa wa Benin, huku mechi hiyo ilishuhudia mipira ya kros 24, ambapo Benin ilipiga krosi 11 na Botswana 13. Botswana ilijiona ina mkosi kwa kushindwa kusawazisha bao hilo baada ya kushudia ikigongesha mwamba mara moja.

RABAT, MOROCCO: BAO la kipindi cha kwanza lililofungwa na Yohan Roche lilitosha kuipa Benin ushindi wao wa kwanza kwenye mashindano ya Afcon 2025 baada ya kuichapa Botswana 1-0 katika mchezo wa Kundi D uliofanyika uwanjani Prince Moulay Abdellah Olympic Annex, Jumamosi.

Benin ilihitaji ushindi kwenye mechi hiyo ya pili kwenye kundi lao ili kukusanya pointi za kuweka hai matumaini yao ya kutinga hatua ya mtoano na hilo lilifanikiwa kwa kuichapa Botswana, huku mchezo mwingine wa kundi hilo ulitarajiwa kuzikutanisha Senegal la DR Congo, ambazo zote zilishinda mechi zao za kwanza.

Roche alifunga baada ya shuti lake kumbabatiza kwenye goti beki wa Botswana, lakini alifanya hivyo baada ya asisti maridadi kutoka kwa Steve Mounie. Benin sasa imefikisha pointi tatu, hivyo inasubiri mechi ya mwisho kwenye kundi hilo, ambapo itamenyana na Senegal, ambapo kama itakosa ushindi, basi itahitaji sare ili kujiweka kwenye wakati mzuri wa kufuzu mtoano kwa kupitia timu za tatu bora.

Katika mechi yao dhidi ya Botswana, Benin ilipiga jumla ya mashuti 10, ambapo manne tu ndiyo yaliyolenga folini, huku wapinzani wao walipiga mashuti manne na moja pekee ndilo lililolenga goli. Kwenye umiliki wa mpira, Benin ilifanya hivyo kwa asilimia 53 dhidi ya 47 za Botswana, huku timu zote zikipiga kona moja moja kwa kila upande.

Kipa wa Botswana alifanya sevu tatu, dhidi ya moja ya kipa wa Benin, huku mechi hiyo ilishuhudia mipira ya kros 24, ambapo Benin ilipiga krosi 11 na Botswana 13. Botswana ilijiona ina mkosi kwa kushindwa kusawazisha bao hilo baada ya kushudia ikigongesha mwamba mara moja.