Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Salah, Mahrez wakabana koo

SALAH Pict

Muktasari:

  • Salah na Mahrez kila mmoja amefunga mabao mawili, wanaongoza orodha ya wenye mambo mengi wakiwa sambamba na Lassine Sinayoko wa Mali, Brahim Diaz wa Morocco, Nicolas Jackson wa Senegal na Elias Achouri wa Tunisia.

KABLA ya mechi za leo Jumamosi za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zilizohusisha timu za makundi ya C na D tayari jumla ya mabao 34 yalikuwa yamefungwa katika mechi 16 ikiwa ni wastari wa mabao 2.13 kwa kila mechi, huku nyota wa Algeria Riyad Mahrez na Mohamed Salah wa Misri wakikabana katika orodha ya wafungaji.

Salah na Mahrez kila mmoja amefunga mabao mawili, wanaongoza orodha ya wenye mambo mengi wakiwa sambamba na Lassine Sinayoko wa Mali, Brahim Diaz wa Morocco, Nicolas Jackson wa Senegal na Elias Achouri wa Tunisia.

Hata hivyo, Salah, Sinayoko na Diaz wamefunga mabao yao kupitia mechi mbili kila mmoja tofauti na Mahrez, Jackson na Achouri waliofunga katika mechi moja moja ilizocheza timu zao katika michuano hiyo ya 35 tangu ilipoanzishwa mwaka 1957.

Salah alifunga juzi kwa penalti bao la ushindi dhidi ya Bafana Bafana, baada ya awali kufunga bao la ushindi pia dhidi ya Zimbabwe katima mechi za Kundi B, kama ilivyokuwa kwa Sinayoko na Diaz ambao kila mmoja alifunga penalti katika mechi ya Kundi A iliyoisha kwa sare ya 1-1.

SALA 01

Awali Sinayoko alifunga pia bao katika sare ya 1-1 dhidi ya Zambia na Diaz alifungwa wakati Morocco ikiifunga Comoros kwa mabao 2-0.

Kwa upande wa Mahrez alifunga mabao mawili wakati wanaizamisha Sudan kwa mabao 3-0, huku Jackson akifunga mabao mawili Senegal ilipoifumua Botswana pia kwa mabao 3-0 na Achouri alifunga pia mabao yake wakati Tunisia ikiitambia Uganda kwa mabao 3-1.

Hata hivyo, Jackson na Achouri walikuwa na nafasi ya kuongeza idadi ya mabao jana Jumamosi kwani kila mmoja alikuwa uwanjani kucheza mechi za raundi ya pili zilizohusisha mechi za Kundi C na D.

Tunisia ilitarajiwa kuvaana usiku na Nigeria, huku Senegal ilitarajiwa kucheza mapema alasiri dhidi ya DR Congo.

SALA 02

Kabla ya mechi za jana jumla ya kadi nyekundu tatu zimeshatolewa katika michuano hiyo wakipewa Basilio Ndong wa Guinea ya Ikweta, Saleheldin Al Hassan wa Sudan na Mohamed Hany wa Misri, huku jumla ya penalti tano zikitolewa katika mechi hizo 15, tatu zikifungwa na mbili kukoswa.

Wachezaji walikosa penalti ni Soufiane Rahimi wa Morocco dhidi ya Comoros na El Bilal Toure wa Mali dhidi ya Zambia, wakati Mohamed Salah, Sinayoko na Diaz kila mmoja akitupia nyavuni.