Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DR Congo haijuti kumwacha Yoane Wissa

WISSA Pict

Muktasari:

  • Kocha Sebastien Desabre amesema ulikuwa uamuzi mgumu na Wissa alisikitishwa kutoshiriki mashindano hayo Morocco, lakini kutokuwepo kwake kulikuwa kwa masilahi ya mchezaji mwenyewe na timu ya taifa.

DR Congo imesema haina majuto kuhusu uamuzi wa kumwacha Yoane Wissa nje ya kikosi cha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ikieleza walitaka awe katika hali bora zaidi kwa mechi za mchujo wa fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Machi, mwakani.

Kocha Sebastien Desabre amesema ulikuwa uamuzi mgumu na Wissa alisikitishwa kutoshiriki mashindano hayo Morocco, lakini kutokuwepo kwake kulikuwa kwa masilahi ya mchezaji mwenyewe na timu ya taifa.

Wissa (29), alipata jeraha la goti alipokuwa akiichezea DR Congo dhidi ya Senegal katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia mapema Septemba na alirejea uwanjani wiki tatu zilizopita tu akiwa na klabu yake mpya, Newcastle United, kama mchezaji wa akiba katika ushindi wao dhidi ya Burnley.

WIS 01

Tangu wakati huo, ameingia akitokea benchi mara mbili katika Ligi Kuu ya England (EPL) na alianza na kufunga bao katika ushindi wa robo fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Fulham wiki iliyopita, jambo lililoibua swali iwapo DR Congo ilijutia uamuzi wa kutomchagua kwa AFCON.

“Tuliendelea kuwasiliana kwa karibu na madaktari wa Newcastle kwa miezi kadhaa na tukafanya uamuzi wa kufuata taratibu za kitabibu kwa umakini na kutomuwekea shinikizo la kurejea mapema,” Desabre amesema katika mkutano na waandishi wa habari juzi Ijumaa kabla ya mechi ya Kombe la Mataifa dhidi ya Senegal iliyopigwa jana Jumamosi huko Tangier.

“Nilichukua uamuzi wa mwisho wa kumwacha (nje ya kikosi cha AFCON) ili apate nafasi bora kabisa ya kupona vizuri, kwa sababu tunamhitaji akiwa katika kiwango chake bora.

“Ulikuwa uamuzi mgumu na najua amesikitishwa kutokuwepo hapa na wenzake, lakini anaelewa,” aliongeza kocha huyo wa DR Congo.

DR Congo watacheza dhidi ya Senegal Jumamosi katika mechi yao ya pili ya Kundi D ya Kombe la Mataifa ya Afrika, mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa baada ya timu hizo kukutana katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia miezi mitatu iliyopita.

Senegal waligeuka kutoka nyuma baada ya kufungwa mabao mawili na kushinda DR Congo 3-2 mjini Kinshasa na hatimaye wakafuzu Kombe la Dunia litakalofanyika mwaka ujao nchini Canada, Mexico na Marekani.

WIS 02

Hata hivyo, DR Congo tangu wakati huo waliendelea kushinda mchujo wa Afrika kwa timu zilizomaliza nafasi ya pili mwezi Novemba na sasa wapo mechi moja tu kufuzu pia Kombe la Dunia.

Watacheza dhidi ya Jamaica au New Caledonia Machi kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026.

“Wachezaji wanafurahia sana kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika na labda… labda baada ya miezi sita tutawaona kwenye Kombe la Dunia pia,” aliongeza Desabre.

“Tumefanikisha mengi katika miezi ya karibuni, tukiishinda Cameroon na Nigeria katika mchujo wa Kombe la Dunia na tuna ubora mzuri wa kiufundi katika timu yetu.

“Tumeonyesha kuwa tuna uwezo wa kupata matokeo dhidi ya timu bora barani Afrika.”