Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misri yatangulia mtoano Afcon 2025

MISRI Pict

Muktasari:

  • Misri sasa imefikisha pointi sita baada ya mechi mbili, hivyo ina uhakika wa kumaliza kwenye nafasi mbili za juu kwenye kundi. Afrika Kusini imebaki na pointi tatu baada ya mechi mbili, wakati Zimbabwe na Angola zenyewe kila moja ina pointi moja baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mapema.

AGADIR, MOROCCO: MKWAJU wa penalti uliopigwa na Mohamed Salah kwenye kipindi cha kwanza umeisaidia Misri iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kuichapa Afrika Kusini 1-0 katika mchezo wa Kundi B uliofanyika Agadir, Ijumaa na hivyo kuwa taifa la kwanza kutinga hatua ya mtoano kwenye mashindano ya Afcon 2025.

Misri sasa imefikisha pointi sita baada ya mechi mbili, hivyo ina uhakika wa kumaliza kwenye nafasi mbili za juu kwenye kundi. Afrika Kusini imebaki na pointi tatu baada ya mechi mbili, wakati Zimbabwe na Angola zenyewe kila moja ina pointi moja baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mapema.

Salah aliyesababisha penalti hiyo baada ya kupigwa kofi usoni na beki wa Afrika Kusini, Khuliso Mudau akiwa ndani ya boksi na baada ya picha za VAR iliamriwa kupigwa penalti na kumfanya staa huyo wa Liverpool kufunga bao lake la pili kwenye mashindano hayo ya Afcon 2025.

Misri ilimpoteza beki wake wa kulia Mohamed Hany baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza na hivyo kuifanya Afrika Kusini kushambulia sana kwenye kipindi cha pili na nusura ipate penalti kama si VAR kugoma.

Angola na Zimbabwe zilipata pointi zao za kwanza, lakini kwa matokeo hayo ya sare ya 1-1 wote wamejiweka kwenye hatari ya kutupwa nje ya mashindano. Timu hizo mbili zilipoteza mechi zao za kwanza za Kundi B na hivyo zimebakiza mechi moja, ambapo Zimbabwe itakipiga na Afrika Kusini na Angola itamalizana na Misri.

Afrika Kusini ilipiga mashuti 16, saba yalilenga golini kwenye mechi hiyo dhidi ya Misri, ambayo ilipiga mashuti saba, huku matatu tu ndiyo yaliyolenga goli.

Kipa wa Misri alifanya sevu sita katika mechi ambayo Afrika Kusini ilipiga pasi 536, ambapo za mbele zilikuwa 155 na kurudisha mpira nyuma zilikuwa 64, huku ikipiga pasi ndefu 47 na krosi 28. Misri ilipiga pasi 308, ambapo pasi za mbele zilikuwa 118 na za nyumba 46, huku pasi ndefu zilikuwa 57 na kupiga krosi 11.

MSIMAMO ULIVYO KUNDI B AFCON 2025

                       P         W        D         L         GF          GA          PTS

Misri               2         2         0          0          3              1              6

A. Kusini         2         2         0         2          2              2              3

Zimbabwe      2         0        1         1           2              3              1

Angola            2         0        1         1           2               3              1