Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa wamefunika mechi za kwanza AFCON 2025

AFCON Pict

Muktasari:

  • Shughuli ya mapema kabisa ilikuwa baina ya Angola na Zimbabwe, kisha ikafuatia Misri na Afrika Kusini, kabla ya Zambia kukipiga na Comoro na Morocco wenyeji kumalizana na Mali. Kilichotokea, kimetokea.

RABAT, MOROCCO: KWENYE Boxing Day kulipigwa mechi nne za Afcon 2025, zilizokuwa za pili kwenye makundi wakati vigogo wa soka la Afrika walipoonyesha ubabe uwanjani kujaribu kufahamu hatima zao za kutinga raundi inayofuata kwenye mashindano.

Shughuli ya mapema kabisa ilikuwa baina ya Angola na Zimbabwe, kisha ikafuatia Misri na Afrika Kusini, kabla ya Zambia kukipiga na Comoro na Morocco wenyeji kumalizana na Mali. Kilichotokea, kimetokea.

Mambo ni moto. Mchakamchaka huo utaendelea Jumamosi, kwa mechi nyingine nne na Benin itakamuana na Botswana, Senegal na DR Congo, wakati Tanzania itaulizana maswali magumu na majirani zao Uganda, huku Nigeria ikimaliza ubishi na Tunisia. Utamu uko hapo. Ukizubaa imekula kwako.

AFC 01

Afcon 2025 imekuwa na mambo matamu kwa kuwapata burudani ya kutosha mashabiki na kwenye mechi za kwanza za makundi, hakukuwa na mechi yoyote iliyomalizika kwa matokeo ya kuboa, hakukuwa na timu iliyomalizika kwa 0-0.

Kwenye mechi zote za Afcon 2025 za kwanza kwenye hatua ya makundi, mashabiki walinyanyuka kutoka vitini kushangilia mabao, nyavu hazikulala njaa. Mechi za pili kwenye makundi, zilianza Ijumaa ya Boxing Day. Ilikuwaje? Ulijionea.

AFC 02

Baada ya kuona mechi za kwanza za makundi, timu zote zinazopewa nafasi kubwa ya kunyakua taji hilo kuanza kwa Misri na Senegal hadi kwa Algeria na Morocco zote zimeonyesha ubabe wao kwenye mechi zao za kwanza Afcon 2025.

Na katika mechi hizo za kwanza za makundi, kuna wachezaji walionyesha viwango vya hali ya juu na kunyakua tuzo za Wachezaji Bora wa Mechi, huku Manchester United ikitamba kwa kutoa wachezaji wawili, Bryan Mbeumo wa Cameroon na Amad Diallo wa Ivory Coast, waliobeba tuzo za Wachezaji Bora wa Mechi kwenye hiyo Afcon 2025 Matchday 1. Mambo ni moto.


AFC 03

HII HAPA ORODHA YA WACHEZAJI BORA WA MECHI AFCON 2025 - DAY 1

-Morocco 2–0 Comoros: Brahim Díaz (Morocco)

-Mali 1–1 Zambia: Lassine Sinayoko (Mali)

-Afrika Kusini 2–1 Angola: Lyle Foster (Afrika skuini)

-Misri 2–1 Zimbabwe: Omar Marmoush (Misri)

-DR Congo 1–0 Benin: Théo Bongonda (DR Congo)

-Senegal 3–0 Botswana: Nicolas Jackson (Senegal)

-Nigeria 2–1 Tanzania: Semi Ajayi (Nigeria)

-Tunisia 3–1 Uganda: Elias Achouri (Tunisia)

-Burkina Faso 2–1 Equatorial Guinea: Edmond Tapsoba (Burkina Faso)

-Algeria 3–0 Sudan: Riyad Mahrez (Algeria)

-Ivory Coast 1–0 Msumbiji: Amad Diallo (Ivory Coast)

-Cameroon 1–0 Gabon: Bryan Mbeumo (Cameroon)