Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Emiliano Martinez kumrithi Becker Liverpool

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa Martinez ambaye msimu huu amecheza mechi 49 za michuano yote,  unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na kwa mujibu wa watu wake wa karibu anatamani sana kuondoka ili kupata changamoto mpya.

LIVERPOOL inadaiwa kumfuatilia kipa wa Aston Vila na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez, 33, ili akawe mbadala wa kipa wao Alisson Becker anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Martinez ni mmoja wa makipa bora kwa sasa katika EPL na alikuwa akihusishwa kuondoka dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwenda Manchester United kabla ya dili hilo kufeli katika dakika za mwisho za dirisha la usajili.

Mkataba wa Martinez ambaye msimu huu amecheza mechi 49 za michuano yote,  unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na kwa mujibu wa watu wake wa karibu anatamani sana kuondoka ili kupata changamoto mpya.

Mbali ya Liverpool, saini ya Martinez pia inawindwa na Juventus na Inter Milan za Italia ambazo bado hazijaanza mazungumzo ya kumsajili.

Kwa mujibu wa taarifa, mabosi wa Villa wapo tayari kumwachia staa huyu aende lakini wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.

Kiasi hicho cha pesa kinatajwa ndio kinazirudisha nyuma timu nyingi ambazo zinaonekana ni kikibwa sana ukilinganisha na umri wake.


Joao Gomes

ARSENAL na Manchester United zinaonekana kuwa zina asilimia chache ya kupata nafasi ya kumsajili kiungo wa Wolves na timu ya taifa ya Brazil, Joao Gomes, 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza Gomes yuko karibu kufikia makubaliano na Atletico Madrid ambayo yeye ndio chaguo lake kwa sasa.

Kiungo huyo amekuwa akiwindwa na vigogo wengi barani Ulaya kutokana na uwezo wake, pia ameshaweka wazi hatoendelea kusalia Wolves kwa msimu ujao baada ya timu hiyo kushuka daraja.


Josko Gvardiol

BAYERN Munich na Real Madrid zimewasiliana na wawakilishi wa beki wa kimataifa wa Croatia, Josko Gvardiol, kuhusu uwezekano wa kumsajili staa huyo wa Manchester City.

Hata hivyo, mabosi wa Man City hawaonekani kuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo kuondoka kirahisi, hivyo dili lolote litakalotokea linaweza kuiingizia zaidi ya Pauni 70 milioni kama ada ya uhamisho.

Kwa mujibu wa  ripoti, kwa sasa Man City inafanya mazungumzo na wakala wake kwa ajili ya kumsainisha dili jipya ili kuzivunja nguvu kabisa timu zinazomnyemelea.


Ethan Nwaneri

ARSENAL ipo tayari kumuuza mshambuliaji wao wa  kimataifa wa England, Ethan Nwaneri, 19, dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza Chelsea ni miongoni klabu zinazomfuatilia kwa karibu kijana huyo mwenye kipaji kikubwa.

Nwaneri, ambaye ametokea akademi ya Arsenal, amekuwa akitajwa kutaka kuondoka Arsenal tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.


Luka Vuskovic

INAELEZWA beki wa Tottenham Hotspur, Luka Vuskovic, 19, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo  Hamburger SV, anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo msimu ujao baada ya kiwango chake kuimarika sana akiwa huko Ujerumani.

Awali, uongozi wa Spurs ulikuwa unafikiria kumuiuza staa huyu mazima lakini Vuskovic amezidi kuonyesha kiwango bora siku hadi siku kiasi cha kuwafanya vigogo hao wasitishe mpango wao wa kwanza. Licha ya kuonyesha nia ya kurudi Tottenham, beki huyo pua ana ofa kutoka kwa timu kadhaa Ulaya.


Robin Roefs

CHELSEA imeanza kufanya mazungumzo ya kutaka kumsajili kipa wa Sunderland, Robin Roefs, 23, ili akawe mbadala wa kipa wao wa sasa, Robert Sanchez ambaye bado ameendelea kufanya makosa mengi yanayoigharimu timu.

Roefs ni moja ya nguzo muhimu sana za Sunderland ambayo imekuwa katika mwenendo mzuri msimu licha yakuwa ndio imepanda daraja.

Sanchez amekuwa akihusishwa kuondoka tangu mwaka jana, sababu kubwa ikitajwa ni benchi la ufundi kutokuwa na imani naye kwa sababu anafanya sana makosa.


Jhon Lucumi

SUNDERLAND inaonekana kuwa katika hatua nzuri kumsajili beki wa Bologna, Jhon Lucumi, 27, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa benchi la ufundi la Sunderland linahitaji sana huduma ya staa huyu ambaye ilijaribu kutaka kumsajili dirisha lililopita la majira ya baridi lakini ikashindikana.

Lucumi ndiye beki kiongozi wa Bologna, lakini amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara. Msimu huu amecheza mechi 35 za michuano yote.


Jannik Schuster

BRENTFORD ipo katika harakati za kukamilisha usajili wa beki wa Red Bull Salzburg na Austria, Jannik Schuster, 19, dirisha lijalo.

Inaripotiwa dili hilo linaweza kufikia thamani ya Pauni 17 milioni kiasi ambacho Salzburg imesisitiza hakipungui.

Schuster ni mmoja wa wachezaji vijana wanaochipukia na amezivutia klabu kadhaa kutokana na uwezo wake na utulivu akiwa na mpira mguuni.