Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hispania yaitupa nje Austria, ikifuzu 16 bora

SPAIN Pict

Muktasari:

  • Hispania imepata bao hilo likifungwa na mshambuliaji Mikel Oyarzabal akimalizia krosi nzuri ya beki wa kushoto, Marc Cucurella mwenye kasi ya kupandisha mashambulizi.

Hispania imeweka hesabu zake sawa, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Austria kwenye mchezo uliokuwa mkali kwa timu zote mbili.

Haikuwa rahisi kwa Hispania kupata ushindi huo ambapo imewalazimu kusubiri kwa dakika 36 kupata bao la kwanza ikikutanana na ubora wa safu ya ulinzi ya Austria.

Hispania imepata bao hilo likifungwa na mshambuliaji Mikel Oyarzabal akimalizia krosi nzuri ya beki wa kushoto, Marc Cucurella mwenye kasi ya kupandisha mashambulizi.

Oyarzabal bao hilo lilikuwa la tatu kwake kwenye fainali hizo za mwaka huu ambapo mpaka mapumziko, Hispania ikatoka na uongozi wa bao 1-0.

Kipindi cha pili, Hispania ikaendelea kutafuta mabao zaidi ikilishambulia kwa nguvu lango la Austria huku kipa Alexander Schlager akiendelea kuonyesha ubora.

Dakika ya 61, Austria ikapoteza nafasi nzuri ya kufunga kwa kichwa cha mshambuliaji Sasa Kalajdzic, mpira ukapaa juu kidogo akipokea krosi kutoka upande wa kushoto.

Hispania ikapata bao la pili dakika ya 66 likifungwa na beki Pedro Porro kwa kichwa akipokea krosi nzuri ya mshambuliaji Alex Baena.

Msumari wa tatu ukapatikana dakika ya 89, mfungaji akiwa Oyarzabal, akimalizia asisti ya Cucurella na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-0.

Oyarzabal ambaye mechi ya kwanza hatua ya makundi dhidi ya Cape Verde aliweka rekodi ya kucheza dakika 30 za kwanza bila ya kuguda mpira, hivi sasa amekuwa na makali akifikisha mabao manne, mawili nyuma ya vinara Lionel Messi na Kylian Mbappe.

Hispania baada ya kufuzu hatua ya 16 bora, sasa inasubiri kucheza dhidi ya mshindi kati ya Ureno na Croatia, katika kusaka nafasi ya kwenda kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya pili baada ya 2010, fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini.