Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool kukipiga Tottenham Carabao Cup

CARABAO Pict

Muktasari:

  • Katika michezo mingine, Manchester United itamenyana na Brighton & Hove Albion, wakati mabingwa watetezi Manchester City watakuwa wenyeji wa Norwich City.

LONDON, ENGLAND: LIVERPOOL imepangwa kukutana na Tottenham Hotspur katika raundi ya tatu ya Carabao Cup, huku timu tisa za Ligi Kuu England zinazoshiriki michuano ya Ulaya zikianza kampeni zao katika hatua hiyo.

Katika michezo mingine, Manchester United itamenyana na Brighton & Hove Albion, wakati mabingwa watetezi Manchester City watakuwa wenyeji wa Norwich City.

Arsenal itasafiri kucheza na Ipswich Town, huku Aston Villa ikikabiliana na Coventry City.

Timu nyingine zitakazokutana ni Crystal Palace dhidi ya Middlesbrough, Sunderland dhidi ya Hull City na Bournemouth dhidi ya Lincoln City.

Timu zote tisa za Ligi Kuu zinazoshiriki mashindano ya Ulaya msimu huu  Arsenal, Aston Villa, Bournemouth, Brighton, Crystal Palace, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Sunderland  zimeanza Carabao Cup moja kwa moja kutoka raundi ya tatu.

Ili kuepusha mgongano wa ratiba na hatua za mwanzo za Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League, michezo hiyo itachezwa katika wiki zinazoanza Jumatatu, Septemba 7 na Jumatatu, Septemba 14.

Mechi mbili za mwisho za raundi hiyo zitaamuliwa Alhamisi, Chelsea itakapomenyana na Luton saa 1:30 usiku, huku Fulham ikicheza na AFC Wimbledon saa 2:00 usiku.


Droo kamili ya raundi ya tatu

Crystal Palace vs Middlesbrough

Manchester United vs Brighton

Manchester City vs Norwich

Sunderland vs Hull City

Ipswich Town vs Arsenal

Coventry City vs Aston Villa

Bournemouth vs Lincoln City

Liverpool vs Tottenham

Chelsea au Luton vs Leeds United

Millwall vs Newcastle United

Fleetwood Town vs Sheffield United

Everton vs Wolverhampton Wanderers

Leyton Orient vs Bradford City

Reading vs Brentford

Peterborough United vs Barnsley

West Ham United vs Fulham au AFC Wimbledon