Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nicolas Jackson sasa anukia Newcastle

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Newcastle inapambana kuweka sawa safu yao ya ushambuliaji ambayo bado haijapata uwiano sawa tangu kuondoka kwa Alexander Isak.

NEWCASTLE United ni moja ya klabu zinazoiwania saini ya mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya  Senegal, Nicolas Jackson mwenye umri wa miaka 24.

Jackson anatarajiwa kurejea Chelsea dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya  Bayern Munich anayoichezea kwa mkopo msimu huu kuthibitisha hawamsainisha mkataba wa moja kwa moja.

Newcastle inapambana kuweka sawa safu yao ya ushambuliaji ambayo bado haijapata uwiano sawa tangu kuondoka kwa Alexander Isak.

Jackson mwenyewe inadaiwa kuwaambia wawakilishi wake hana mpango tena wa kucheza Chelsea hivyo, anahitaji kujiunga na timu nyingine hata kwa mkopo baada ya Bayern kuamua kutoendelea naye.

Akiwa na Bayern ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Ujerumani msimu huu, Jackson amecheza mechi 39 za michuanbo yote na kufunga mabao 10.

Mkataba wake wa sasa na Chelsea unatarajiwa kumalizika mwaka 2033, na matajiri hao wa Jiji la London wanahitaji zaidi ya Pauni 60 milioni ili kumuuza.


Andy Robertson

ATLETICO Madrid inatarajiwa kuingia kwenye ushindani na Tottenham Hotspur ili kuipata saini ya  beki wa Liverpool na Scotland, Andy Robertson, 32, ambaye amethibitisha kuwa ataondoka katika viunga vya Anfield mkataba wake utakapomalizika Juni mwaka huu ambapo atakuwa mchezanji huru.


Beki huyo wa kushoto amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Liverpool kwa miaka kadhaa, lakini sasa anataka kupata changamoto mpya mahali kwingine baada ya mafanikio aliyoyapata akiwa na majogoo hao.

Atletico inaonekana kuwa ndio ipo katika nafasi kubwa ya kuipata saini ya fundi huyu.


Xavi Simons

MANCHESTER United inafuatilia kwa karibu hali ya kiungo wa Tottenham na Uholanzi, Xavi Simons, 23, ili kumsajili katika lijalo.

Simons ni mmoja wa viungo wenye vipaji kikubwa Ulaya kiasi cha kuivutuia sana Man United ambayo inatazama kwanza hatma ya Spurs itabakia Ligi Kuu England msimu ujao au laa kabla haijawasilisha ofa ya kumsajili.

Man United inapambana kuongeza ubora katika safu yao ya kiungo kuelekea msimu ujao na Xavi anaonekana kuwa sehemu ya mipango yao.


Alisson Becker

LIVERPOOL inajiandaa kwa vita ya kumzuia kuondoka kipa wao namba moja, Alisson Becker, 33, katika dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza kuwa kipa huyo wa kimataifa wa Brazil anaonekana kuwa na mpango wa kuhamia Juventus  ikidaiwa  inahitaji changamoto mpya sehemu nyingine.

Alisson amekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya Liverpool tangu akiwa chini ya Jurgen Klopp na sasa Arne Slot.

Hata hivyo, ikiwa atalazimisha kuondoka, mabosi wa Liverpool hawatosimama na kumzuia.


Bernardo Silva

KIUNGO wa Manchester City na Ureno, Bernardo Silva, 31, yupo katika rada za klabu mbalimbali kubwa Ulaya ikiwemo  Juventus, Barcelona na Paris Saint-Germain zinazohitaji kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Saini ya Silva pia inawindwa sana na  Al-Hilal ya Saudi Arabia ambayo ndio imeweka ofa nono zaidi mezani.

Silva ambaye ameshatangazwa ataondoka City mwisho wa msimu huu, mwenyewe bado anahitaji kuendelea kucheza soka la kiushindani.


John Stones

BEKI wa Manchester City na England, John Stones, 31, ameripotiwa kuwa tayari kujiunga na Barcelona dirisha lijalo la majira ya kiangazi na mkataba wake utakuwa unamalizika.

Stones amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Man City katika miaka ya karibuni, lakini mwisho wa msimu huu, ataondoka ili kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine. Barca imevutiwa sana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali katika safu ya ulinzi.


Yan Diomande

LIVERPOOL imeanza mawasiliano na wawakilishi wa winga chipukizi wa RB Leipzig, Yan Diomande, 19.

Diomande ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora sana, amezichanganya klabu nyingi Ulaya lakini Liverpool inaonekana ndio ya kwanza kuwasiliana na Leipzig ili  kuhakikisha inafikia makubaliano ya kumsajili staa huyo kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia.

Mabosi wa Liverpool wanaamini staa huyu akijiunga nao atakuwa ni biadhaa ya muda mrefu kutokana na umri wake.


Endrick

ARSENAL inamfuatilia mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil, Endrick, 19, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Olympique Lyonnais.

Ripoti zinaeleza Arsenal inaweza kuwasilisha ofa ya kumsajili staa huyu ifikapo mwisho wa msimu lakini kwanza itaulizia uwezekano wa kumpata kwa Madrid yenyewe.

Endrick ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa na Madrid haionekani kuwa tayari kumwachia kwani inaamini anaweza kuwa msaada mkubwa hapo baadae. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2030.


Rumarn Burrell

SUNDERLAND ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England zilizoonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Jamaica, Rumarn Burrell, 25, anayekipiga Queens Park Rangers.

Mbali ya Sunderland, Bournemouth na Wolves ambayo msimu huu imeshuka daraja pia zinahitaji saini yake. Msimu huu amecheza mechi 31 za michuano yote na kufunga mabao 10. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.