Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okoronkwo awashtumu wahudumu wa hoteli kuibia wachezaji

OKORONKO Pict

Muktasari:

  • Okoronkwo, anayekipiga katika AFC Toronto ya Canada, alitoa madai hayo kupitia machapisho kadhaa kwenye akaunti yake ya Snapchat.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria, Esther Okoronkwo ameishutumu hoteli ya Marriott iliyopo jijini Casablanca, Morocco, kwa madai baadhi ya wafanyakazi wake waliiba fedha za wachezaji wa Super Falcons wakati kikosi hicho kikiendelea na maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.

Okoronkwo, anayekipiga katika AFC Toronto ya Canada, alitoa madai hayo kupitia machapisho kadhaa kwenye akaunti yake ya Snapchat.

Alidai wafanyakazi wa usafi waliingia kwenye vyumba vya wachezaji wakati walipokuwa nje na kuiba fedha zilizokuwa kwenye pochi zao.

OKORO 01

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amesema alipoteza Dola 700, huku jumla ya fedha zote zilizoibiwa na wachezaji wengine ni takribani Dola 1,000.

Pia aliwataja baadhi ya wachezaji wenzake ambao walidaiwa kuathirika na tukio hilo ni beki Osinachi Ohale, aliyedaiwa kupoteza Dola 100, kiungo Joy Omewa (Dola 120), nahodha Rasheedat Ajibade (Dola 200) na kiungo Halimatu Ayinde (Dola 100).

OKORO 02

Okoronkwo amesema "Hoteli hii ya Marriott mjini Casablanca imeiba fedha nyingi kutoka kwenye pochi za watu kadhaa."

"Wameiba Dola kutoka kwa mchezaji mwenzangu. Wafanyakazi wa usafi ndio waliochukua fedha hizo. Walisubiri hadi tulipotoka vyumbani ndipo wakaingia kusafisha na kuiba pesa."

Okoronkwo pia amesema wachezaji hao hawakuridhishwa na namna uongozi wa hoteli ulivyoshughulikia malalamiko yao baada ya kuripoti tukio hilo.

OKORO 03

"Tulianza kuzungumza nao, lakini hawakuwa na majibu yoyote. Badala yake, walianza kutuonyesha kutokuwa na heshima," amesema.

Licha ya  Okoronkwo kutoa malalamiko hayo mitandaoni hadi sasa si Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) wala hoteli hiyo iliyotoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

Mabingwa hao watetezi wataanza kampeni yao ya kutetea taji hilo Julai 28 wakiikaribisha Malawi mechi itakayopigwa Uwanja wa Al Madina uliopo Rabat.