Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Diop: Senegal tunaitaka fainali

DIOP Pict

Muktasari:

  • Hii ni mara ya nne Senegal inafuzu WAFCON na mwaka 2012 ilipoishia hatua ya makundi, mwaka 2022 na 2024 mara mbili mfululizo ikiishia hatua ya robo fainali.

MSHAMBULIAJI wa Senegal, Mama Diop amesema mafanikio ya timu ya taifa ya wanaume kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya pili yamekuwa chachu kubwa kwao kuelekea michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON).

Hii ni mara ya nne Senegal inafuzu WAFCON na mwaka 2012 ilipoishia hatua ya makundi, mwaka 2022 na 2024 mara mbili mfululizo ikiishia hatua ya robo fainali.

Diop amesema safari hii lengo lao ni kuvuka hatua ya robo fainali na kufika mbali zaidi ili wavunje rekodi ya matoleo mawili yaliyopita.

Amesema mafanikio ya timu ya wanaume yameongeza ari na kuamini Senegal inaweza kuwa miongoni mwa mataifa makubwa ya soka Afrika kwa pande zote mbili.

"Tulifurahi sana kwa mafanikio yao. Ni fahari kubwa kuona timu ya wanaume ikitwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya pili. Hilo limetupa motisha zaidi kwa sababu sasa matarajio ya watu ni kuona Senegal ikiendelea kufanya vizuri kwenye soka nasi tunataka kufikia kiwango hicho," amesema Diop.

Akizungumzia malengo yao kwenye WAFCON, mshambuliaji huyo amesema siri ya mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu, huku akibainisha kuwa hawaridhishwi tena na kuishia robo fainali kama ilivyokuwa kwenye mashindano yaliyopita.

"Kinachohitajika ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu. Mara ya mwisho tuliishia robo fainali lakini safari hii tunataka kwenda mbali zaidi. Lengo letu ni kuvuka hatua hiyo kufika fainali na kwa nini isiwe hivyo kufuzu kwenye mashindano makubwa zaidi duniani. Hiyo ndiyo ndoto ambayo kila mmoja wetu ndani ya timu anaipigania," amesema.