Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid kusukwa upya kwa Sh60.6 bilioni

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Katika mazingira ya kawaida, hali hii ingeonekana ya kutisha, lakini Madrid ina nafasi ya kufanya maboresho ya haraka na ya gharama nafuu kwenye kikosi cha kwanza huku ikisubiri uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya usajili maalum ambao unaweza kuchukua muda kukamilika.

Real Madrid inalazimika kufanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chake. Inaonekana majira haya ya kiangazi yatakuwa ya hekaheka nyingi kwa klabu hiyo, jambo ambalo si rahisi hasa kutokana na hali ya soko la usajili ilivyo kwa miaka ya hivi karibuni. Kufanya mapinduzi ya kikosi kwa kutumia fedha nyingi sasa ni kazi ngumu katika nyakati hizi.

Katika mazingira ya kawaida, hali hii ingeonekana ya kutisha, lakini Madrid ina nafasi ya kufanya maboresho ya haraka na ya gharama nafuu kwenye kikosi cha kwanza huku ikisubiri uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya usajili maalum ambao unaweza kuchukua muda kukamilika.

Wachezaji wakubwa wanaweza kuchelewa kuwasili, lakini wakati huo huo kuna mipango mingine rahisi, lakini yenye manufaa makubwa.

Mpango wa timu kwa msimu ujao unaathiri karibu nusu ya kikosi. Dani Carvajal na David Alaba wataondoka klabuni mikataba yao itakapomalizika. Mkataba wa Antonio Rudiger pia unaisha msimu huu wa kiangazi na bado hajaongeza mkataba mpya. Dani Ceballos bado ana mkataba lakini kuondoka kwake kunaonekana kuwa jambo la uhakika.

Gonzalo García yupo mbioni kuondoka kutokana na sababu za kimkakati za kisoka, huku kukiwa na nia ya kumuuza Raul Asencio. Hatma ya Franco Mastantuono bado haijulikani, hali kadhalika kwa Fran Garcia.

Zaidi ya hayo, Eder Militao, Ferland Mendy na Rodrygo ni maswali makubwa kutokana na majeraha ya muda mrefu yaliyolazimisha Madrid kujiandaa vizuri zaidi.

Kana kwamba haitoshi, pia kuna uwezekano wa kuuza mchezaji mkubwa, huku Eduardo Camavinga akiwa kwenye mjadala mkubwa.

Kwa kifupi, tayari kuna wachezaji wawili wanaoondoka rasmi na wengine 10 wakiwa katika hali tofauti zinazotia mashaka mustakabali wao.


Ibrahima Konate

Beki Ibrahima Konate anatarajiwa kuondoka Liverpool baada kuichezea timu hiyo kwa miaka mitano ndani ya Anfield.

Beki huyo mwenye miaka 27 alikuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya lakini hakufikia makubaliano na klabu hiyo, hivyo sasa anatarajiwa kuondoka bure.

Konate alijiunga na Liverpool akitokea RB Leipzig katika majira ya kiangazi ya mwaka 2021. Ameichezea klabu hiyo mechi 183 na kushinda taji moja la Ligi Kuu England, FA Cup moja na mawili ya Carabao. Bado hajafanya uamuzi kuhusu hatua yake inayofuata.


Piero Hincapie

Piero Hincapie anaonekana yupo karibu kujiunga moja kwa moja na Arsenal FC baada ya kukamilisha mkataba wake wa mkopo akitokea Bayer Leverkusen, huku Barcelona wanaonekana wanaweza kuharibu dili hilo.

Barcelona wanafikiria kufanya usajili wa Hincapie msimu huu wa kiangazi. Arsenal walimsajili beki huyo kwa mkopo msimu uliopita, huku mkataba huo ukiwa na kipengele cha kununua kwa pauni milioni 45.

Hata hivyo, Arsenal bado hawajathibitisha kama watatumia kipengele hicho kitakachomfanya mchezaji huyo wa Ecuador kusaini mkataba wa miaka mitano.

Kutokana na hali hiyo, Barcelona wanaangalia uwezekano wa kumsajili wakitafuta beki mpya wa kati anayependelea upande wa kushoto.


Robert Lewandowski

Mshambuliaji Robert Lewandowski anaweza kuelekea Marekani baada ya kuondoka Barcelona. Kocha wa Chicago Fire FC, Gregg Berhalter, amethibitisha hadharani kuwa klabu hiyo ina nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Poland mara tu atakapomaliza muda wake Barcelona.

Berhalter amesema wazi kuwa tayari wamekuwa na mazungumzo na nyota huyo na klabu hiyo inafanya kila iwezalo kumshawishi kuhamia Major League Soccer.

“Ninaweza kuzungumza wazi kwa sababu si mchezaji wa Barcelona tena, au hivi karibuni hatakuwa tena, na ni mmoja wa wachezaji tunaotaka kuwaleta,” amesema Berhalter.


Angel Gomes

Nyota mpya wa timu ya taifa ya England, Angel Gomes anatakiwa kwa nguvu zote naNewcastle United.

Hata hivyo, kocha Eddie Howe anakabiliwa na ushindani kutoka Liverpool, Tottenham Hotspur FC na Borussia Dortmund kwa ajili ya kiungo huyo wa zamani wa Manchester United FC ambaye sasa anacheza Lille.

Klabu kadhaa zilimfuatilia Gomes alipong’ara katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Finland kwenye UEFA Nations League.


Matt O’Riley

Tottenham Hotspur FC wanajiandaa kufanya usajili wa kiungo wa Brighton & Hove Albion FC, Matt O’Riley, katika dirisha hili. Vyanzo vimeeleza kuwa Tottenham wanaendelea kumfuatilia nyota huyo wa Denmark, lakini Atlético Madrid na Borussia Dortmund ndio wanaoonekana kuwa mbele zaidi kwenye mazungumzo.

Brighton wako tayari kusikiliza ofa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25, huku ikielezwa kuwa hatakuwa sehemu ya mipango ya kocha Fabian Hurzeler baada ya muda wake wa mkopo akiwa Marseille.


Marcos Senesi

Tottenham wako karibu kumsajili beki wa AFC Bournemouth, Marcos Senesi, kwa uhamisho wa bure. Makubaliano binafsi bado hayajakamilika, lakini dili la mchezaji huyo mwenye miaka 29 linaendelea vizuri.

Pia Spurs wanaendelea na mpango wa kumsajili beki wa pembeni wa Scotland, Andy Robertson, ambaye amemaliza mkataba wake na kuondoka Liverpool.

Bournemouth walikata tamaa ya kumbakisha Senesi baada ya kukataa ofa ya tatu ya mkataba mpya mwezi Desemba na kuanza mazungumzo na klabu kubwa za nje ya England.


Andoni Iraola

Bayer Leverkusen wako katika mazungumzo ya hatua za mwisho za kumteua Andoni Iraola kuwa kocha wao mpya. Kocha huyo wa zamani wa Bournemouth anahitajika baada ya kuiongoza timu hiyo kufuzu UEFA Europa Ligi.

Crystal Palace FC pia wameonyesha nia ya kumchukua Iraola kuwa kocha wao mpya. Hata hivyo, inaelezwa kuwa ni vigumu kwake kujiunga na mabingwa wa UEFA Europa Conference Ligi kutokana na mazungumzo yanayoendelea na Leverkusen.

Crystal Palace bado wanaendelea kutafuta kocha mpya baada ya Oliver Glasner kuondoka klabuni msimu huu.