Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yakoleza moto kumng'oa Rogers Villa

Muktasari:

  • Rogers amekuwa katika kiwango bora tangu msimu uliomalizika, ambapo aliiwezesha timu yake kubeba ubingwa wa Europa League katika kipindi ambacho baadhi ya nyota kikosini walishuka ubora wao. 

SIKU chache baada ya kutangazwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal, wameendelea kupambana usiku na mchana kuhakikisha kwamba wanainasa saini ya kiungo-mshambuliaji wa Aston Villa, Morgan Rogers, 23, katika dirisha la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Ulaya wiki ijayo.

Rogers amekuwa katika kiwango bora tangu msimu uliomalizika, ambapo aliiwezesha timu yake kubeba ubingwa wa Europa League katika kipindi ambacho baadhi ya nyota kikosini walishuka ubora wao. 

Katika kuhakikisha kwamba mpango huo unafanikiwa Arsenal wamekuwa wakiongeza nguvu katika harakati za kumsajili mchezo huyo hasa baada ya msimu kumalizika kutokana na timu nyingi Ulaya kuonyesha nia ya kumsajili, ambapo Barcelona, Atletico Madrid na Real Betis za Hispania zimeanza kutajwa, huku AC Milan na Inter Milan zikihusishwa naye.

Hata hivyo, uwezekano wa kuinasa saini ya mchezaji huyo unaweza kuwa mgumu, baada ya Aston Villa kudaiwa kuanzisha mazungumzo chinichini ili kuuongeza mkataba wake unaotarajiwa kumalizika Juni 30, 2031. Mchezaji huyo amefunga mabao 10 na asisti saba Ligi Kuu England msimu uliomalizika.


Anthony Gordon

BAYERN Munich na Barcelona zinatajwa kuhusishwa na winga wa Newcastle United, Anthony Gordon katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi, huku mabingwa hao wa Ujerumani, Bayern, wakiripotiwa kuwa tayari kwenye mazungumzo na timu yake, ilhali Barca ikijivuta.

Gordon amevutia timu nyingi ambazo zinadaiwa kupishana makao makuu ya St. James' Park kufuatilia iwapo zinaweza kuipata saini yake kwa ajili ya msimu ujao. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika Juni 2030.


Bradley Barcola

WINGA wa Paris Saint-Germain, Bradley Barcola, ni nyota mwingine anayehusishwa na uhamisho kwenda Liverpool kama mrithi anayepaswa kuziba pengo la Mohamed Salah na pia kama mbadala wa Yan Diomande iwapo timu hiyo itashindwa kumnasa wakati dirisha lijalo la usajili.

Barcola amekuwa akihusishwa na timu nyingi Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha PSG kwa misimu ya karibuni na pia uamuzi wa waajiri wake hao kufungua milango kwa timu zinazomtaka.


Joe Gomez

ASTON Villa, AC Milan na Besiktas wanamwania beki wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Joe Gomez mwenye umri wa miaka 29 ili kuinasa saini yake dirisha la usajili lijalo litakapofunguliwa. Gomez amekuwa katika ubora wake msimu huu licha ya kwamba kikosini namba kuipata imekuwa changamoto. Ndani ya Liverpool mchezaji huyo amejikuta akipambania kupenya kikosini na hivyo kumfanya afikirie zaidi kuondoka.


Carlos Baleba

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, anawania wachezaji watatu kutoka klabu yake ya zamani ya Brighton akimtaka kiungo wa Cameroon, Carlos Baleba mwenye miaka 22, beki wa Uholanzi Jan Paul van Hecke, 25, na kipa wa Uholanzi Bart Verbruggen mwenye miaka 23. Spurs pia wanamfikiria beki wa England, John Stones mwenye miaka 31. Uamuzi wa De Zerbi unalenga kuboresha kikosi hicho ambacho kimeponea chupuchupu kushuka daraja Ligi Kuu England.


Jack Grealish

KIUNGO wa kimataifa wa England, Jack Grealish, huenda akapewa nafasi nyingine ya kuonyesha ubora katika kikosi cha Manchester City, ikielezwa kwamba huo ndiyo mpango wa kocha Enzo Maresca ambaye anahusishwa kuchukua mikoba ya Pep Guardiola. Maresca anataka kumpa nafasi Grealish mwenye miaka 30 nafasi ya kufufua kiwango baada ya msimu wa mkopo akiwa Everton, ambako alikuwa chaguo la kwanza. Mkataba wake Man City unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.


Said El Mala

BRENTFORD wamewasilisha ofa ya Pauni 39 milioni kwa ajili ya winga wa kimataifa wa Ujerumani na FC Koln, Said El Mala mwenye umri wa miaka 19. El Mala amekuwa katika kiwango bora na anachukuliwa kuwa mmoja wa nyota wa Kijerumani wanaochipukia kwa kasi katika misimu ya karibuni, ambaye msimu huu amecheza mechi 34 na kufunga mabao 13, huku akitoa asisti tatu katika Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga). Mkataba wake Koln unaisha Juni 30, 2030.


Aaron Wan-Bissaka

BEKI wa kimataifa wa DR Congo na West Ham United, Aaron Wan-Bissaka, 28, anatarajiwa kuzivutia timu nyingi Ulaya hasa baada ya kklabu yake kushuka Ligi Kuu England msimu uliomalizika. Tayari Tottenham Hotspur, Newcastle United, Fulham na Sunderland zimeonyesha nia ya kupambania saini yake kwa ajili ya msimu ujao. Nyota huyo wa zamani wa Manchester United anamaliza mkataba West Ham ifikapo Juni 30, 2031.