Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vipers yaiduwaza Gor Mahia ikifuzu nusu fainali Kagame 2026

Muktasari:

  • Gor Mahia imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa mabingwa wa Uganda, Vipers SC, katika mechi ya pili ya Kundi A iliyochezwa leo Jumatatu, Julai 27, 2026.

Mwanzo mzuri wa Gor Mahia katika michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026, umekatizwa kwa namna ya kusikitisha baada ya kufungwa dakika za mwisho na Vipers SC katika mchezo wao wa pili wa Kundi A.

Gor Mahia imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa mabingwa wa Uganda, Vipers SC, katika mechi ya pili ya Kundi A iliyochezwa leo Jumatatu, Julai 27, 2026.

Awali, Gor Mahia ilianza kampeni yao kwa kishindo ikiichapa APR FC ya Rwanda mabao 5-0 katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa Ijumaa, Julai 24, 2026 kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali. Mechi ya pili imepoteza 1-0 dhidi ya Vipers.

Katika mechi ya leo, Gor Mahia ilitawala dakika 15 za mwanzo, ikionyesha pasi za kuvutia na mashambulizi ya mara kwa mara, lakini ilikwama mbele ya safu imara ya ulinzi ya Vipers SC.

Kwa upande wa Vipers SC, ilicheza soka la nguvu na kutumia mabavu katika kuzuia mashambulizi ya Gor Mahia, hali iliyosababisha baadhi ya wachezaji wa K'Ogalo kuangushwa mara kadhaa.

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mrefu mwanzoni mwa mchezo, Gor Mahia ililazimika kukabiliana na mbinu hizo za Vipers huku ikisaka bao la kuongoza.

Vipers SC ilikaribia kuvunja mwamba dakika ya 23, lakini safu ya ulinzi ya Gor Mahia ilisimama imara na kuokoa hatari hiyo kwa kuruhusu kona, ambayo wageni ilishindwa kuitumia.

Katika shambulizi la kushtukiza lililofuata, Gor Mahia walipoteza mpira na kutoa faulo nje kidogo ya eneo la hatari, lakini Vipers SC nao ilishindwa kuitumia nafasi hiyo.

Vipers SC ilitengeneza tishio lingine dakika ya 32, lakini mabeki wa Gor Mahia walifanya kazi nzuri ya kuondoa hatari kabla haijawa kubwa.

Kipindi cha pili kilipoanza, Gor Mahia ilionekana yenye dhamira ya kubadili mwelekeo wa mchezo baada ya Vipers SC kutawala dakika 45 za kwanza.

Hata hivyo, Vipers SC ilizima haraka kasi hiyo kwa mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na pasi sahihi kutoka eneo la ulinzi, jambo lililoifanya K'Ogalo kubaki chini ya presha.

Kadri kipindi cha pili kilivyoendelea, timu zote zilifanya juhudi za kusaka bao la ushindi, lakini mchezo ulijikita zaidi katikati ya uwanja huku nafasi za wazi za kufunga zikiwa chache.

Licha ya Gor Mahia kufanya mabadiliko na kuingiza wachezaji wapya, hakuna upande ulioweza kuvunja ukuta wa mwenzake.

Gor Mahia iliendelea kushambulia kwa nguvu kuelekea dakika ya 84, huku Vipers SC ikibaki kutengeneza hatari kupitia mashambulizi ya kushtukiza, lakini hakuna timu iliyoweza kupata bao la ushindi hadi kufikia dakika 90.

Wengi wakidhani mechi ingeisha bila bao, hatimaye, Vipers SC ikavunja ngome ya Gor Mahia dakika ya 90+3 kwa kufunga bao la ushindi, hivyo kujihakikishia ushindi wa 1-0 pamoja na kufuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali ikiwa timu ya kwanza kufanya hivyo ikitokea kundi A.

Gor Mahia itamalizia hatua ya makundi kwa kuivaa FC Garde Républicaine ya Djibouti katika mchezo wa mwisho wa Kundi A utakaochezwa Alhamisi, Julai 30, 2026.

Ili Gor Mahia ifuzu nusu fainali, inahitaji kushinda mechi ya mwisho, kisha isikilizie matokeo ya timu zingine zitakazomaliza nafasi ya pili kutoka Kundi B na C kuwania best looser moja.