Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakali wa kila idara ligi tano bora Ulaya

LAMINE Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa inayosikiliziwa kumalizika ni Ligi Kuu England inayomalizika wikiendi hii, Jumapili, Mei 24, 2026 kabla ya mastaa kugeukia fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazopigwa kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, katika nchi za Mexico, Marekani na Canada.

LONDON, ENGLAND: LIGI kuu tano bora barani Ulaya zinaanza kutamatika wikiendi hii, lakini kinachoeleweka tayari ni kwamba nne kati ya hizo zina mabingwa ikiwamo ile ya Hispania (LaLiga) ambako Barcelona wamebeba ndoo, Ufaransa (Ligue 1) kuna PSG, huku Bayern Munich wakiwa wa kwanza kubeba mapema kule Ujerumani, ilhali Italia (Serie A) kukiwa na Inter Milan.

Kwa sasa inayosikiliziwa kumalizika ni Ligi Kuu England inayomalizika wikiendi hii, Jumapili, Mei 24, 2026 kabla ya mastaa kugeukia fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazopigwa kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, katika nchi za Mexico, Marekani na Canada.

Lakini, wakati mambo yakitarajiwa kuhitimika wiki hii kuna mastaa katika ligi hizo wenye wastani mzuri na wa kushangaza katika mambo mbalimbali wanayofanya viwanjani ambayo kwa ujumla yamewafanya kuteka mijadala katika ulimwengu wa soka.

LAMI 03

UFUNGAJI MABAO

Licha ya kwamba Harry Kane wa Bayern Munich ndiye kinara wa mabao kwa ujumla hadi sasa katika ufungaji kwenye ligi hizo akiwa na mabao 36 akifuatiwa na Erling Haaland (Man City) 26 huku Kylian Mbappe (Real Madrid) akitupia 24, lakini wastani wake wa kufunga sio mzuri sana ikilinganishwa na Haaland linapokuja suala la muda anaotumia kufunga, hususan katika mchezo wa wazi (open play) akiwa na wastani wa alama 10.79 tofauti na Kane aliye na 9.7.

Hata hivyo, Kane yupo vizuri katika mabao ya penalti ambapo ana wastani wa kufunga kwa asilimia 100 msimu huu ambapo amefunga 14 katika mashindano yote. Wafungaji hao bora wanafuatiwa na Lautaro Martinez wa Inter Milan mwenye mabao 17, akiwa na wastani wa pointi 7.8 huku Esteban Lepaul wa Stade Rennes ya Ligue 1 akitupia mabao 20 huku akishika nafasi ya mwisho na alama 6.4.

LAMI 02

MASHUTI MENGI

Achana na msimu mbaya wa 2025/26 anaoendelea kuwa nao Mbappe, lakini anakimbiza kwa namba si mchezo.

Nyota huyo anakimbiza pia kwa wastani bora wa kupiga mashuti mengi langoni mwa wapinzani msimu huu akiwa na wastani wa pointi 11.2, akifuatiwa na staa mwenzake wa Real Madrid, Vinicius Jr mwenye 9.7 wanaofuatiwa na Khvicha Kvaratskhelia wa PSG mwenye 8.2 huku Julian Alvarez akiwa na wastani wa 7.4 na Harry Kane akishika nafasi ya mwisho katika orodha kwa 6.8.

LAMI 01

WAKALI WA ASISTI

Kando na watupia mabao hao kuna wakali wa kutoa asisti ambao kwa wastani bora wa kila mchezo anayefunika katika kazi hiyo ni Michael Oliseh wa Bayern Munich mwenye wastani wa alama 10.1 akifuatiwa na Bruno Fernandez wa Manchester United (9.7), Lamine Yamal wa Barcelona 9.3, Luis Diaz (Bayern Munich) 8.5 na Julian Alvarez wa Atletico Madrid (6.2).

LAMI 04

MAFUNDI WA PASI

Katika kundi hili mkali wao ni Vitinha wa PSG mwenye wastani wa pointi 9.6 akifuatiwa na Aleksandar Pavlovic wa Bayern Munich mwenye 9.2 huku nyota mwenzake kikosini Joshua Kimmich akiwa nazo 9.0. Watatu wanaofunga kazi ni William Pacho wa PSG na Aleix Garcia wa Leverkusen na Anthony Gordon wa Newcastle United wenye 7.7.