Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bafana Bafana yaipigia hesabu Misri AFCON 2025

Muktasari:

  • Bafana na Mafarao wa Misri wote walishinda mechi zao za ufunguzi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola na Zimbabwe mtawalia, ingawa ushindi huo haukuwa wa kuridhisha kama zilivyotarajia.

BAFANA Bafana ina matumaini ya kuendeleza mwanzo mzuri katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 itakapokutana na Misri katika mechi ya pili wa Kundi B itakayochezwa Agadir kesho Ijumaa. Kwa namna nyingi, huu utakuwa mtihani mkubwa wa uwezo wa ubingwa kwa timu zote mbili.

Bafana na Mafarao wa Misri wote walishinda mechi zao za ufunguzi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola na Zimbabwe mtawalia, ingawa ushindi huo haukuwa wa kuridhisha kama zilivyotarajia.

Sasa zinakutana katika mechi ambayo huenda ikaamua mshindi wa nafasi ya kwanza katika kundi hilo na kwa atakayeshinda, kama mshindi atapatikana, ushindi huo utakuwa nyongeza kubwa ya kujiamini.

Hata hivyo, kuna takwimu moja ya kutisha ambayo itawatetemesha mashabiki wa Bafana kabla ya mechi hiyo.

Imepita miaka 21 na mechi 21 za hatua ya makundi tangu Bafana Bafana walipoifunga Benin katika mechi ya ufunguzi wa Afcon 2004. Tangu wakati huo, imefanikiwa kuifunga mara mbili tu katika hatua ya makundi.

Ukimwuliza shabiki yeyote wa Bafana kama hilo linawezekana, bila shaka atashangaa, hata kwa kuzingatia matatizo mengi ambayo timu imekuwa nayo kwa miaka ya hivi karibuni.

Lakini ukweli ni kwamba ushindi pekee walioupata katika michezo ya makundi tangu hapo ni mara mbili dhidi ya Angola (2013 na 2025) na Namibia (2019 na 2023).

Katika kipindi hicho, imekutana na timu 13 tofauti na imeshindwa kuzifunga timu 11 kati hizo.

Kumekuwa na sare saba na vipigo 10, idadi ambayo ni kubwa mno ya matokeo mabaya katika hatua ambayo kwa kawaida huchukuliwa kuwa rahisi zaidi ya mashindano.

Haijawahi kupata ushindi wa mfululizo katika michezo ya makundi katika kipindi hicho (kwa hakika, ushindi dhidi ya Benin ulikuwa mara ya mwisho walipofanya hivyo), ingawa ushindi mkubwa zaidi katika hatua ya makundi ulitokea kwenye toleo la mwisho walipoiadhibu Namibia kwa mabao 4-0.

Hata hivyo, rekodi hii mbaya ilianza na kipigo chao kikubwa zaidi kuwahi kutokea, kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Nigeria mwaka 2004.

Pamoja na hayo, bado kuna imani kuwa kizazi hiki cha Bafana cha mwaka 2025, ambacho kimekua na kuwa timu yenye ushindani, mapambano na ustadi mkubwa, kinaweza kubadilisha simulizi hii. Ikiwa si dhidi ya Misri ambapo sare itakuwa matokeo mazuri basi hakika katika mechi ya ya mwisho wa kundi dhidi ya Zimbabwe Desemba 29.

Kwa kuangalia rekodi ya jumla ya mechi za makundi tangu ushiriki wa kwanza uliofanikiwa mwaka 1996, takwimu zinaonyesha uwiano wa kati. Bafana Bafana imepata ushindi mara 11, imefungwa mara 11 na kutoka sare mara 12 katika mechi 34, ikifunga mabao 37 na kuruhusu mabao 34.

Katika kipindi hicho, imeweka nyavu safi (cleansheet) mara 12 na pia imeshindwa kufunga mabao katika mechi 12.