Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona kuitingisha Bayern Munich ikimtaka Harry Kane

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Barcelona wameweka kipaumbele kusajili mshambuliaji msimu huu wa joto kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa kati wa Poland, Lewandowski, 37, anayeondoka na wamewaweka katika orodha nahodha wa England na Bayern Munich, Kane, 32; mshambuliaji wa Argentina anayekipiga  Atletico Madrid, Julian Alvarez, 26, pamoja na straika wa Brazil wa Chelsea, Joao Pedro, 24.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Harry Kane yupo kwenye orodha fupi ya Barcelona ili kwenda kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski anayeondoka.

Barcelona wameweka kipaumbele kusajili mshambuliaji msimu huu wa joto kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa kati wa Poland, Lewandowski, 37, anayeondoka na wamewaweka katika orodha nahodha wa England na Bayern Munich, Kane, 32; mshambuliaji wa Argentina anayekipiga  Atletico Madrid, Julian Alvarez, 26, pamoja na straika wa Brazil wa Chelsea, Joao Pedro, 24.

Hata hivyo, dili la kumpata Kane linahitajika kuwa kubwa kutokana na Bayern kuendelea kutamani kubaki naye kikosini ikizingatiwa kwamba amekuwa katika mazungumzo ya kuboresha mkataba wake unaotarajiwa kuwa na nyongeza nono zaidi ya maslahi.

Vilevile kuna hofu kwamba Barcelona inayokumbana na wakati mgumu kutokana na matatizo ya kifedha inaweza kuishia kumtamani tu mchezaji huyo kwani hata yeye hajaonyesha nia ya kutaka kuachana na Bayern Munich. Barca iliwahi kumsajili Lewandowski kutoka Bayern Munich.


Ederson

MANCHESTER United inadaiwa kukubaliana dili la Pauni milioni 46 kwa ajili ya usajili wa kiungo wa Brazil, Ederson Jose dos Santos Lourenco da Silva maarufu Ederson, 26, kutoka Atalanta. Ederson alikuwa anaonekana kwenda Atletico Madrid, lakini klabu hiyo ya Hispania inapendelea kiungo mwingine wa Brazil, Joao Gomes, 25, anayekipiga Wolverhampton Wanderers ambaye pia yupo kwenye rada ya Manchester United.


Samuel Martinez

LIVERPOOL inafanyia kazi dili la kumchukua nyota anayechupukia wa Colombia, Samuel Martinez, 17, kutoka Atletico Nacional, ikipambana kuipiku Barcelona na Borussia Dortmund katika mbio za kumsajili kiungo huyo mshambuliaji. Kwa sasa bado hakuna uhakika iwapo itafanikiwa kwa sababu kumekuwapo na vita kutoka timu mbalimbali ambazo pia zinamfukuzia mchezaji ahuyo anayeng’ara kwa sasa nchini kwao.


John Stones

EVERTON watakutana na ushindani kutoka Bayern Munich katika kuwania saini ya beki wa England, John Stones, 31, ambaye atakuwa huru baada ya mkataba wake na Manchester City kumalizika katika msimu huu. Beki huyo ambaye amekuwa akikumbana na wakati mgumu kupata namba Man City ameitwa katika kikosi cha England kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026 na hivyo huenda likampandisha thamani yake.


Victor Munoz

WINGA wa Osasuna, Victor Munoz, 22, ameingia katika rada za Newcastle United ambayo imejiunga na Aston Villa katika mbio za kumuwania staa huyo wa kimataifa wa Hispania. Iwapo dili lake litakamalika atakwenda kuwa mbadala wa nyota wa kimataifa wa England, Anthony Gordon, 25, anayetarajiwa kuhamia Bayern Munich. Hata hivyo, dila la Munoz linaweza kukumbana na wakati mgumu kutoka timu zingine.


Jonathan David

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Canada, Jonathan David, 26, anayeichezea Juventus anafukuziwa na Newcastle United, Aston Villa, Leeds United, Brighton na Crystal Palace ambapo zote zimeshaelezwa kuhusu upatikanaji wake. Kwa sasa kinachosubiriwa ni ofa kuwasilishwa mezani, lakini vita miongoni mwa timu hizo huenda ikawa kubwa mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa. Mkataba wake Juventus unaisha 2030.


Ousmane Diomande

BOURNEMOUTH wanapanga dili la kushtukiza la kumchukua beki wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast, Ousmane Diomande, 22, kutoka Sporting CP kama mbadala wa beki wa Kiargentina Marcos Senesi, 29, ambaye ataondoka klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2030.


Mason Greenwood

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Mason Greenwood anayekipiga Marseille pamoja na winga wa Uholanzi, Crysencio Summerville wa West Ham United wote wakiwa na umri wa miaka 24 wako katika mipango ya kunyakuliwa na Roma. Greenwood ameanza kukumbana na wakati mgumu Marseille ambako kiwango chake kimeanza kushuka na hivyo mashabiki kuzomewa na mashabiki.