Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makundi Fainali za Kombe la Dunia 2026 haya hapa

Muktasari:

  • Katika droo hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri, ilifanyika baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kupokea Tuzo ya Amani ya FIFA ya kwanza.

Droo ya Fainali za Kombe la Dunia 2026, imefanyika Ijumaa ya Desemba 5, 2025 katika Ukumbi wa Kennedy uliopo mjini Washington nchini Marekani.

Katika droo hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri, ilifanyika baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kupokea Tuzo ya Amani ya FIFA ya kwanza.

Fainali hizo zitakazochezwa katika nchi za Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11, 2025 hadi Julai 19, 2025, zitashirikisha mataifa 48, yakipangwa kwenye makundi 12, kila kundi likiwa na timu nne.

Hadi sasa, mataifa 42 yamejihakikishia kushiriki fainali hizo, yakibaki sita yanayosubiri kucheza mechi za mchujo zitakazofanyika Machi 2026.

Katika mchujo huo, mataifa mawili yatafuzu kupitia mchujo wa FIFA na manne yakitumia mchujo wa Ulaya.

Mchujo wa Ulaya una mataifa 16 yaliyogawanywa katika makundi manne, kila kundi linatoa mshindi mmoja.

Kundi A lina Wales, Bosnia and Herzegovina, Italia na Northern Ireland.  

Kundi B kuna Ukraine, Sweden, Poland     na Albania.        

Kundi C linaundwa na Slovakia, Kosovo, Uturuki na Romania.         

Kundi D ni Czech Republic, Republic of Ireland, Denmark na North Macedonia.

Mchujo wa FIFA nafasi ya kwanza kuna New Caledonia, Jamaica na DR Congo, wakati nafasi ya pilu zipo Bolivia, Suriname na Iraq.

Baada ya droo kufanyika, Marekani, miongoni mwa nchi mwenyeji imepangwa kundi D ikiwa na Australia, Paraguay na mshindi wa mchujo wa Ulaya C (Uturuki, Romania, Slovakia na Kosovo).

Canada ambayo nayo ni nchi mwenyeji, ipo kundi B pamoja na Uswizi, Qatar na mshindi wa Mchujo wa Ulaya A (Wales, Bosnia and Herzegovina, Italia na Northern Ireland).

Mwenyeji mwingine Mexico yupo kundi A na Afrika Kusini, Korea Kusini na mshindi wa Nafasi ya Mchujo wa Ulaya D (Czech Republic, Republic of Ireland, Denmark na North Macedonia).

Kumbuka upangaji wa makundi ulifanywa kwa kuzingatia hakuna timu mbili kutoka shirikisho moja zitakutana hatua hii isipokuwa Ulaya pekee.


MAKUNDI RASMI YA KOMBE LA DUNIA 2025 YAPO HIVI

Kundi A: Mexico, Afrika Kusini, Korea Kusini na mshindi wa Nafasi ya Mchujo wa Ulaya D

Kundi B: Canada, mshindi wa Nafasi ya Mchujo wa Ulaya A, Qatar, Uswisi

Kundi C: Brazil, Morocco, Haiti, Scotland

Kundi D: Marekani, Paraguay, Australia, mshindi wa Nafasi ya Mchujo wa Ulaya C

Kundi E: Ujerumani, Curaçao, Ivory Coast, Ecuador

Kundi F: Uholanzi, Japan, mshindi wa Nafasi ya Mchujo wa Ulaya B, Tunisia


Kundi G: Ubelgiji, Misri, Iran, New Zealand

Kundi H: Hispania, Cape Verde, Saudi Arabia, Uruguay

Kundi I: Ufaransa, Senegal, mshindi wa Nafasi ya Pili wa Mashindano ya Mchujo ya FIFA, Norway

Kundi J: Argentina, Austria, Algeria, Jordan

Kundi K: Ureno, mshindi wa Mashindano ya Mchujo ya FIFA 1, Colombia, Uzbekistan

Kundi L: England, Croatia, Ghana, Panama