Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford atua katika rada za Tottenham

Muktasari:

  • Taarifa zinaeleza kuwa Spurs imeingia katika mchakato huo baada ya kuona Barcelona inasuasua kumsainisha mkataba wa moja kwa moja staa huyo ambaye kwa sasa anacheza katika kikosi hicho kwa mkopo.

TOTTENHAM Hotspur imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, 28, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Taarifa zinaeleza kuwa Spurs imeingia katika mchakato huo baada ya kuona Barcelona inasuasua kumsainisha mkataba wa moja kwa moja staa huyo ambaye kwa sasa anacheza katika kikosi hicho kwa mkopo.

Rashford bado ni mmoja kati ya washambuliaji wenye uwezo mkubwa na msimu huu akiwa kwa mkopo Barca ameonyesha kiwango bora akifunga mabao 13 katika mechi 45 za michuano yote.

Hadi sasa bado hakuna mwafaka wowote uliofikiwa kati ya Barca na wawakilishi wa Manchester ambao wanahitaji Pauni 26 milioni ili kumuuza mazima staa huyo. Hata hivyo, Barca haionekani kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa na badala yake inataka kupunguziwa au ikishindikana ipewe tena kwa mkopo.


Victor Osimhen

MKURUGENZI wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, alisafiri hadi Istanbul, Turuki, Jumapili iliyopita kufuatilia mchezo wa Galatasaray dhidi ya Fenerbahce ikiwa ni katika harakati za kumfuatilia mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen, 27. Osimhen anachukuliwa kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora , Ulaya kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao na Arsenal inataka kumsajili katika dirisha lijalo ili kuboresha eneo lao ushambuliaji.

Awali mabosi wa Arsenal walikuwa na mpango wa kumsajili Julien Alvarez lakini sasa nguvu zao zinaonekana kuhamia kwa Osimhen ambaye hakuna uhakika wa asilimia 100 ikiwa Galatasaray itakuwa tayari kumwachia.


Anthony Gordon

INAELEZWA kuwa kuna uwezekano mkubwa winga wa Newcastle United na England, Anthony Gordon, 25, akaondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Gordon amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwa Newcastle kwa muda mrefu, lakini vigogo wengi Ulaya wamekuwa wakihitaji saini yake hali inayomfanya hata mchezaji mwenyewe kushawishika kuondoka. Man United ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumsajili.


Nathan Ake

EVERTON inajiandaa kumsajili beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi, Nathan Ake, 31, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa kuwa Ake anatafuta muda zaidi wa kucheza, jambo linalomfanya kufikiria kuondoka Man City ambako ushindani safu ya ulinzi ni mkubwa. Kwa upande wa Everton, inaamini uzoefu wa Ake EPL kucheza nafasi nyingi safu ya ulinzi utakuwa nyongeza muhimu katika kikosi chao.


Yan Diomande

LIVERPOOL inaamini uhusiano mzuri na RB Leipzig unaweza kusaidia kumsajili mapema winga chipukizi wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yan Diomande, 19, katika dirisha la majira ya kiangazi. Liverpool imekuwa ikifanya dili mbalimbali na Leipzig na pia kocha wake wa zamani Jurgen Klopp kwa sasa ni miongoni mwa viongozi wa kampuni inayomiliki timu hiyo, hivyo inaamini inaweza kumpata.


Maxi Araujo

NEWCASTLE United na Aston Villa zimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Uruguay, Maxi Araujo, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Araujo ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja akicheza kama winga na beki wa kushoto. Klabu zote mbili zimeanza mazungumzo na wawakilishi wake, lakini hadi sasa hakuna hata moja iliyowasilisha ofa rasmi kwenda kwa Lisbon ili kumsajili.


Dani Olmo

MANCHESTER City, PSG na Arsenal zipo katika vita kuwania saini ya kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Dani Olmo, 27. Taarifa kutoka Barca zimefuchua kuwa mabosi wa timu hiyo wapo tayari kumuuza Olmo ikiwa watapokea ofa nono mwisho wa msimu. Olmo ambaye ni zao la akademi ya Barcelona, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2030.


Christian Kofane

ARSENAL inaendelea kumfuatilia kwa karibu mshambuliaji kijana wa kimataifa wa Cameroon, Christian Kofane, 19, anayekipiga katika kikosi cha Bayer Leverkusen. Inaelezwa Leverkusen inahitaji hadi Pauni 60 milioni ili kumuuza mchezaji huyo katika dirisha la majira ya kiangazi. Kofane kwa sasa ni mmoja kati mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Leverkusen na mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029.