Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yafungua milango dili la Camavinga, Liverpool yatajwa

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa sasa wa Camavinga unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na tangu kuanza msimu huu amecheza mechi 37 za michuano yote, amefunga mabao mawili na kutoa asisti moja.

REAL Madrid inapanga kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi dirisha lijalo la  majira ya kiangazi na kiungo wao wa kimataifa wa Ufaransa, Eduardo Camavinga, 23, ni miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuondoka, huku timu kadhaa za England ikiwemo Liverpool zimeonyesha nia ya kumsajili.

Camavinga, ambaye ni mmoja wa viungo wenye kipaji kikubwa Ulaya, amekuwa akitumika katika nafasi mbalimbali Madrid, lakini mabadiliko ya kimkakati yanaweza kumfanya kuwa sehemu ya wachezaji watakaotolewa.

Hata hivyo, licha ya kuwa tayari kumuuza kiungo huyu, ripoti zinadai Madrid itahitaji zaidi ya Euro 80 milioni ili kumruhusu.

Mkataba wa sasa wa Camavinga unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na tangu kuanza msimu huu amecheza mechi 37 za michuano yote, amefunga mabao mawili na kutoa asisti moja.

Mabosi wa  Liverpool wanataka kusuka upya pia kikosi chao kwa msimu ujao baada ya kufanya vibaya msimu huu na inadaiwa kutaka kuachana na kundi kubwa la wachezaji.


Morgan Rogers

Mshambuliaji wa Aston Villa, Morgan Rogers, 23, yupo katika rada za Bayern Munich, ambayo imejitosa katika vita dhidi ya Chelsea  na Manchester United kuiwania saini ya staa huyo.

Rogers ni mmoja wa wachezaji muhimu Villa kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali za safu ya ushambuliaji. Klabu nyingi zinaamini anaweza kuwa faida kubwa na akatumika kwa muda mrefu kutokana na umri alionao sasa.

Hata hivyo, Villa hawatarajiwi kumuachia kirahisi nyota wao huyo, hivyo klabu yoyote itakayomtaka italazimika kutoa ofa kubwa ili kufanikisha dili hilo.


Curtis Jones

KIUNGO wa Liverpool na England, Curtis Jones, 25, anajiandaa kuondoka Anfield dirisha lijalo la  majira ya kiangazi. Aston Villa inatajwa kuwa tayari kuongeza juhudi zao ili kuhakikisha inampata kiungo huyo ambaye inamwona kama nyongeza muhimu. Jones amekuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kwa muda mrefu, lakini ushindani mkubwa wa nafasi unadaiwa kumfanya hata yeye kutafuta changamoto mpya ili kupata muda zaidi wa kucheza. Iwapo dili hilo litakamilika, Aston Villa inaweza kuongeza ubunifu na nguvu mpya.


Tino Livramento

MANCHESTER City inaendelea kumpa kipaumbele beki wa Newcastle United, Tino Livramento, 23, kama chaguo lao kuu katika orodha ya mastaa inaotaka kuwasajili dirisha hili.

Livramento amekuwa kivutio kwa klabu nyingi kubwa Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu na mbali ya kuwa na uwezo mkubwa wa kukaba, pia anasaidia timu katika kushambulia.

Mkataba wa Livramento unamalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 24 za michuano yote.


Benjamin Nygren

CELTIC inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 26 milioni ili kumuuza winga wao wa kimataifa wa Sweden, Benjamin Nygren, 24, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Nyota huyo ambaye anawindwa sana na Tottenham Hotspur, yupo tayari kujiunga na wababe hao lakini anataka kusubiri kwanza kuona ikiwa itabakia Ligi Kuu au laa.

Mbali ya Spurs, huduma ya fundi huyu pia inahitajika na Brighton, Bournemouth na Valencia.


Marco Palestra

LIVERPOOL inadaiwa kutaka kutuma wawakilishi wake kwenda Italia kwa ajili ya kuzungumza na Atalanta juu ya uwezekano wa kuwauzia Marco Palestra, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Cagliari akitokea Atalanta.

Palestra ambaye anacheza kama beki wa kulia ameendelea kuonyesha kiwango bora kwa msimu huu hali iliyowavutia maskauti wengi wa timu kubwa za Ulaya ambao wamekuwa Italia kumtazama staa huyo akicheza katika mechi kadhaa.


Karim Coulibaly

NEWCASTLE United inafanya mazungumzo na wawakilishi wa  beki chipukizi wa Werder Bremen na timu ya taifa ya  Ujerumani chini ya miaka 21, Karim Coulibaly, 18.

Coulibaly, ameonekana kuwa mmoja kati ya mabeki bora katika Bundesliga kwa sasa kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu  licha ya umri wake mdogo jambo lililozivutia timu nyingi.

Mbali ya Newcastle, Bayern Munich nayo pia inahitaji huduma ya fundi huyu na ipo tayari kulipa hadi Euro 30 milioni kuhakikisha inakamilisha dili lake.


Aurelien Tchouameni

LIVERPOOL bado inaendelea kumfuatilia kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Aurelien Tchouameni, 26, anayekipiga katika kikosi cha Real Madrid.

Inaelezwa awali Manchester United pia ilikuwa ikihitaji huduma ya staa huyu lakini sasa imeamua kujitoa na kuiacha Liverpool pekee. Hata hivyo,

Madrid haionekani kuwa na mpango wa kumuuza fundi huyo licha ya kutopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi chao cha kwanza.