Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zambia, Nigeria mzigoni WAFCON

MZIGONI Pict

Muktasari:

  • Katika Uwanja wa Rabat Olympic, Zambia itaanza kampeni yake dhidi ya Misri majira ya saa 12:00 jioni, huku bingwa mtetezi Nigeria akishuka kwenye dimba la Al Medina saa 3:00 usiku.

BAADA ya kushuhudia kufunguliwa kwa mechi za kundi A na B za fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) leo ni zamu ya kundi C na mechi mbili zitapigwa kwenye viwanja tofauti jijini Rabat.

Katika Uwanja wa Rabat Olympic, Zambia itaanza kampeni yake dhidi ya Misri majira ya saa 12:00 jioni, huku bingwa mtetezi Nigeria akishuka kwenye dimba la Al Medina saa 3:00 usiku.

Mechi ya kwanza inaonekana kuwa ya wazi zaidi kwa Zambia, ambayo ni moja ya timu zinazotarajiwa kufanya vizuri kwenye mashindano haya. Copper Queens wanaongozwa na nyota hatari Barbra Banda na Racheal Kundananji, huku wakibeba rekodi ya kumaliza nafasi ya tatu WAFCON 2022 na kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake 2023.

Misri inaingia ikiwa haitabiriki, lakini takwimu zinaipa Zambia nafasi kubwa zaidi kwa sababu ya mafanikio yao ya hivi karibuni. Kitakachowasaidia kwenye mechi hiyo ni nidhamu ya ulinzi, uzoefu wa baadhi ya wachezaji na uwezo wa kucheza bila presha kwa sababu hawabebwi na matarajio makubwa kama ilivyo kwa Copper.

MZIG 01

Misri wanarejea WAFCON baada ya kukosa mashindano yaliyopita  na wanabebwa zaidi na historia kuliko ubora wa sasa wa kikosi. Wachambuzi wanaipa Zambia nafasi kubwa ya kuondoka na pointi tatu kutokana na uzoefu, kasi ya safu ya ushambuliaji na ubora wa kikosi chao.

Mechi nyingine itawakutanisha Nigeria bingwa mtetezi anayeanza safari ya kutetea taji lake dhidi ya Malawi ambao ni wageni kwenye michuano hiyo. Super Falcons ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya WAFCON ikiwa imetwaa taji hilo mara 10, huku ikiwa haijawahi kupoteza mechi ya kwanza ufunguzi wa mashindano hayo kwa zaidi ya miongo miwili.

Malawi ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza WAFCON, wanakuja wakiwa na morali kubwa wakitamba na safu bora ya ushambuliaji inayoongozwa na Tabitha na Temwa Chawinga ambao ni ndugu, lakini uzoefu wa Nigeria katika michuano mikubwa unaifanya iwe timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

MZIG 02

Kwa mara ya kwanza Malawi inaingia WAFCON ikiwa na safu ya ushambuliaji yenye wachezaji wanaocheza katika kiwango cha juu kwenye ligi mbalimbali duniani. Dada hao wawili wamekuwa tishio kubwa kwa timu nyingi kutokana na uwezo wao wa kubadilisha mchezo muda wowote.

Thabitha ni moja ya majina ya kuchungwa kwenye mechi hiyo kwani ana rekodi mbalimbali akiwa na akiwa na Wuhan Jianghan University ya China alishawahi kuwa mfungaji bora. Msimu wa 2022/23 akiwa na Inter Milan ya Italia alimaliza kinara wa ufungaji akipachika mabao 23 ya ligi akiwa PSG alifunga mabao 19 kabla ya kuhamia Lyon.

Mdogo wake Temwa akiwa na Kansas City ya Marekani alitwaa tuzo ya Golden Boot baada ya kufunga mabao 20 msimu wake wa kwanza 2024. Alikuwa miongoni mwa wachezaji bora wa NWSL na akashinda tuzo ya MVP ya ligi.

Vilevile akiwa Ligi ya China kwenye klabu ya Wuhan Jianghan University, alifunga zaidi ya mabao 80 kwenye ligi hivyo anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaovunja rekodi ya Nigeria leo.